Author: Ezekiel Kamwaga

AKIANDIKA katika gazeti maarufu nchini Israel la Haaretz hivi karibuni, mwanahistoria maarufu, Yuval Harari, alieleza kwamba katika historia, kuna mapinduzi ya namna mbili; yale ya kutoka juu na mengine ya kutoka chini. Mapinduzi ya kutokea chini ni yale ambayo yamezoeleka zaidi. Mwanajeshi anaongoza kikosi cha askari wenzake kupindua serikali iliyoko madarakani. Au wananchi wanachukua silaha dhidi ya serikali dhalimu na kuiondosha madarakani. Barani Afrika, Asia na Amerika Kusini hili lilikuwa jambo la kawaida katika karne iliyopita. Wananchi wanaamka asubuhi au usiku wa manane na kusikia sauti ya askari wanayemsikia kwa mara ya kwanza akiwaambia serikali imebadilika. Mapinduzi…

Read More

MWAKA 2017, utawala wa Rais John Magufuli ulikuwa umeanza kushika kasi. Wakati huo nilikuwa Mhariri wa gazeti la Kiswahili la kila wiki la Raia Mwema na uchambuzi wangu kuhusu uteuzi wa baraza lake la kwanza la mawaziri – ambapo nilihoji uchache wa Wazanzibari, Waislamu na Wanawake kwenye baraza hilo, ulikuwa tayari umevuruga uhusiano wangu naye. Kwa kifupi, uchambuzi wangu ulieleza kwamba haikuwa sahihi kuwa na baraza la mawaziri lenye wanawake wawili na Wazanzibari wa idadi hiyo katika nyakati hizi ambazo usawa wa kijinsia na kelele kuhusu Muungano  hasa kutoka upande wa Zanzibar, yalikuwa ni masuala tete. Hitimisho langu kuhusu baraza…

Read More