Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
Author: Ezekiel Kamwaga
Picha: Baraza la Kwanza la Mapinduzi Zanzibar WIKI iliyopita mwandishi Salma Said alichangia katika mazungumzo ya humu mtandaoni yaliyoanzishwa na makala ya @ahmedrajab katika Gazeti la Dunia yakimzungumzia Badawi Qullatein. Salma aliandika kuwa yeye aliwahi kukutana na kuzungumza na Badawi. Akawataja pia makomredi wakuu wengine wa Umma Party aliowahi kukutana nao, kwa mfano Ali Sultan Issa, Salim Rashid na Khamis Abdulla Ameir, ambaye Mei Mosi atatimia miaka 93. Salma alituhimiza tukisome kitabu cha Khamis alichokizindua mwaka jana kiitwacho “Maisha yangu: Miaka minane ndani ya Baraza la Mapinduzi. Khaini au Mhanga wa Mapinduzi?” Kitabu hicho kinauzwa ALIFU Bookshop,…
Picha: Marais Julius Nyerere wa Tanganyika na Abeid Amani Karume wakitia saini Hati za Muungano. Na Ezekiel Kamwaga MARA ya kwanza kusikia jina la Misha Feinsilber ilikuwa wakati niliposoma – kwa mara ya kwanza pia, kitabu adhimu cha Harith Ghassany “Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru (2010) ” takribani muongo mmoja uliopita. Mara ya pili ikawa kwenye mahojiano niliyowahi kuyafanya jijini Dar es Salaam na aliyekuwa mke wa mwanasiasa na mwanazuoni nguli wa Kizanzibari, hayati Abdulrahman Omar Babu, Bi Ashura, ambapo jina hilo liliibuka pia. Huyu Misha – wengine wakimwita Mischa, alikuwa nani? Kwa Ghassany alitambulishwa kama mfanyabiashara aliyetoa boti iliyowarejesha Zanzibar…
Picha ya Xi: Kwa hisani ya AP/Andy Wong. Na Mark Leonard KATIKA siku za karibuni, Rais Xi Jinping wa China ametawala vichwa vya habari katika vyombo vya Magharibi kwa matukio makubwa mawili. Mosi ni kwa namna alivyofanikisha mazungumzo baina ya Iran na Saudi Arabia na pili ziara yake nchini Russia ambako alitoa mawazo yake kuhusu namna ya kumaliza vita vya Ukraine. Jarida mashuhuri la The Economist limeeleza matukio haya kuwa yamefungua ukurasa mpya kwa watu kuanza kuifikiria dunia kwa kutumia jicho la Rais huyo wa China. Maneno hayo ya Xi yameleta mtikisiko na fadhaa – Wajerumani wangesema Sturm und Drang, katika nchi…
Na Ezekiel Kamwaga KATIKA sehemu ya kwanza ya makala haya wiki iliyopita, nilitaka kuweka historia kidogo ya nafasi ya Makamu wa Rais tangu mwaka 1995. Hii ni kwa sababu, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 ndiyo ulikuwa wa kwanza ambapo nafasi ya mgombea mwenza (Makamu wa Rais) ilikuwepo. Kabla ya mwaka 1995 – yaani kuanzia mwaka 1990 kushuka chini, hakukuwahi kuwa na mgombea mwenza. Watanzania walikuwa wakienda kupiga kura kuchagua Rais. Nafasi ya Makamu wa Rais kwanza ilikuwa ni ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) baada ya Muungano wa mwaka 1964 na baadaye ikaja kuwa ya Rais wa…
Picha kwa hisani ya mtandao wa Africanintelligence. MACHAFUKO yameanza upya nchini Sudan. Mgogoro wa sasa ni mbaya kwa sababu unahusisha watu wawili wenye silaha – Mkuu wa Majeshi, Jenerali Abdel Fatah al Burhan na Kiongozi wa Vikosi vya Mgambo, Jenerali Mohamed Hamdani Dagalo maarufu kwa jina la Hemedti. Kwangu, huu unaweza kugeuka kuwa mgogoro mbaya zaidi kwa Sudan katika kipindi cha miongo minne iliyopita. Katika siasa za bara la Afrika, migogoro iliyofanya uharibifu mkubwa wa mali na uhai wa watu ni migogoro iliyohusu viongozi wenye majeshi. Majenerali hawa awali walikuwa maswahiba wakubwa kisiasa. Uhusiano wao ulianza mwanzoni mwa miaka ya…
Picha kwa Hisani ya gazeti la serikali la Daily News. KITABIA, nafasi ya Makamu wa Rais katika nchi inayofuata mfumo wa uchaguzi wa Kimarekani – kama ilivyo kwa sehemu hapa kwetu Tanzania, ni nafasi iliyopoa na inayoboa. Enzi nikiwa ripota, mara mbili niliwahi kutumwa na mhariri wangu kwenda kuandika kuhusu mkutano wa mmoja wa Makamu wa Rais waliopita lakini nikaomba kupangiwa sehemu nyingine. Nilijua hakutakuwa na stori. Kwa kawaida, Makamu wa Rais huwa ‘hasemi’ kitu. Kuna sifa nyingine ambayo huwa haisemwi hadharani kuhusu nafasi ya Makamu wa Rais; sifa hiyo ni kwamba kwa vyovyote vile hatakiwi kung’ara kuliko bosi wake.…
Na Ezekiel Kamwaga KUTOKANA na kuimarika kwa mahusiano ya kisiasa baina ya vyama vitatu vikubwa vya siasa nchini Tanzania; Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ACT Wazalendo, maswali yameibuka – nani anapata nini kwenye maridhiano haya ya kisiasa? Ninawafahamu wanasiasa wawili wabunge wa CCM ambao wamezungumza nami wakionesha wasiwasi mkubwa kwamba maridhiano haya yanamaanisha wao kukosa ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Kwao, maridhiano haya hayana faida. Ninawafahamu pia wanasiasa kadhaa wa vyama vya upinzani ambao wanaona vyama vya upinzani – hasa Chadema, vinakosea kwa kuonekana kuwa karibu na chama ambacho kimetumia takribani miaka…
WAZIRI Mkuu mstaafu, Cleopa David Msuya (92), ametoa siri ya namna ya kudumu madarakani na Watanzania pasipo migogoro; kuwaeleza ukweli. Katika mazungumzo yake na Gazeti la Dunia, Msuya alisema jambo kubwa alilojifunza kwenye utumishi wake wa umma uliodumu kwa takribani nusu karne, ni kwamba kama watu wakiambiwa ukweli na kuelewa, viongozi hawatakuwa na kitu cha kuhofia. “Nimejifunza sana kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Mwanzoni mwa miaka ya 1980, tulipitia wakati mgumu sana kiuchumi. Yeye aliita wazee hapa Dar es Salaam na kuwaeleza kwamba hali ni ngumu na tunatakiwa kufunga mikanda. “Wananchi walimsikia Rais wao akisema hivyo na…
Na Willy Mutunga IBARA ya 37 ya Katiba ya Kenya inampa Raila Odinga na Wakenya wengine haki ya kuandamana, kufanya kusanyiko na kufanya shinikizo kwa njia ya amani, bila vurugu au kubeba silaha. Kwenye mazingira ya namna hii, wajibu wa kikatiba wa vyombo vya dola wakati wa maandamano ni kuhakikisha kuwa haki hiyo ya Raila na Wakenya wote “inatimizwa, kulindwa na kuheshimiwa”. Hii maana yake ni kwamba kazi ya Polisi, kwa mfano, ni kutoa ulinzi kwa waandamanaji “kwa usalama na bila kutumia silaha” kama ilivyo kwa watu wengine ili Wakenya wafurahie haki yao hiyo ya kikatiba. Ni…
HALI ya kiafya ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa, inaelezwa kuwa ya kutoridhisha katika siku za karibuni na kwamba sasa “anapigania uhai wake”, Gazeti la Dunia linaweza kuthibitisha. Lowassa anayetarajiwa kutimiza umri wa miaka 70 Agosti 26 mwaka huu, amelazwa nchini Afrika Kusini alikopelekwa mwanzoni mwa mwaka jana kwa matibabu zaidi baada ya awali kutibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Taarifa za karibuni kutoka kwa wanafamilia na marafiki wa karibu zimeeleza kwamba kwa sasa mwanasiasa huyo mashuhuri yuko hospitalini katika uangalizi maalumu kwenye Wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU) huko Afrika Kusini . “Mimi sina cha kukwambia kwa sasa.…
