Author: Ezekiel Kamwaga

Maaelezo ya picha: Waziri wa Nishati, January Makamba, akiwa katika mazungumzo na wakuu wa kampuni za Shell na Equinor mnamo Septemba mwaka 2021, siku chache tu baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo.  Na Ezekiel Kamwaga KAMA Tanzania ingekuwa kampuni iliyosajiliwa katika soko la hisa, wiki iliyopita hisa zake zingepanda. Katika masoko yote makubwa ya hisa duniani yakiwamo ya London na New York, hisa za kampuni za Shell, Equinor na Exxon Mobil, ziliongezeka thamani. Kilichosababisha kupanda kwa bei ya hisa hizo kilikuwa ni kufikiwa kwa makubaliano baina ya kampuni hizo na Serikali ya Tanzania…

Read More

Maelezo ya picha: Mgombea wa upinzani katika uchaguzi wa Uturuki, Kemal Kılıçdaroğlu (kushoto), akitembea kwenye mitaa ya Ankara Mei 19 mwaka huu.  Na Murat Sommer na Jennifer McCoy Uchaguzi wa Rais na Wabunge nchini Uturuki uliofanyika Mei 14 mwaka huu ulikuwa mkali huku ukiweka rekodi ya watu kujitokeza kwa wingi kupiga kura. Asilimia 88.9 ya waliojiandikisha walijitokeza kupiga kura; ikimaanisha watu tisa katika kila watu 10 walioandikishwa, walipiga kura. Katika siku za mwisho kuelekea uchaguzi huo, kura za maoni zilikuwa zikimpa ushindi mgombea wa upinzani, Kemal Kılıçdaroğlu, aliyeshindana na Rais wa sasa wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan.…

Read More

Maelezo ya picha: Mwonekano wa Ofisi mpya za Ikulu, Chamwino, Dodoma. Picha kwa hisani ya Ikulu. Na Ezekiel Kamwaga WAKATI unapoingia kwenye eneo ilikojengwa Ikulu mpya ya Chamwino mkoani Dodoma, kuna vitu viwili unaviona haraka; kwanza ni ukubwa wa eneo husika – eneo lina ekari zaidi ya 8,000 na pili ni upekee wa jengo lenye ofisi hizo. Majengo huwa yanazungumza lugha yake na linapokuja suala la mamlaka, ujenzi wa kitu chochote chenye uhusiano na utawala huwa na tabia zake. Profesa Maurice Amutabi aliandika katika andishi lake la mwaka 2016, Colonial Architecture and Urbanism in Africa; “Nyakati za…

Read More

Maelezo ya picha: Mgombea wa chama cha Move Forward, Pita Limjaroenrat, (katikati) akiwashukuru wapiga kura wake kwenye eneo la Mnara wa Demokrasia jijini Bangkok, walipokusanyika kusherehekea ushindi wa chama chao kwenye uchaguzi uliofanyika Mei 15, mwaka huu. Picha kwa hisani ya gazeti la Times la Uingereza.  Na Francesca Regalado, Bangkok VYAMA vya upinzani vimepata ushindi usiotarajiwa katika Uchaguzi Mkuu wa Thailand uliofanyika Mei 15 mwaka huu. Ushindi wa chama cha Move Forward ilikuwa ni kauli thabiti dhidi ya siasa za kujuana na zinazoongozwa na ushawishi wa jeshi la nchi hiyo. Chama hicho kilishinda kwa kufanya kampeni iliyokwenda…

Read More

NENO: Mei 19 mwaka huu, mpigania haki mweusi mashuhuri, Malcolm X, angetimiza miaka 98 endapo angekuwa hai hadi leo. Maisha yake yalikatishwa kikatili kwa kupigwa risasi jijini New York, Marekani, Februari 25, mwaka 1965. Makala hii imechapishwa humu kama sehemu ya kumbukumbu ya maisha yake. Mhariri Maelezo ya picha: Malcolm X (kushoto), akizungumza na aliyekuwa Waziri katika Serikali ya Tanzania, Abdulrahman Babu, ofisini kwa mwanasiasa huyo jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea Tanzania mwaka 1964. Na Ahmed Rajab DESEMBA 3, mwaka 1964, Malcolm X, mwanaharakati wa Kimarekani mwenye asili ya Kiafrika, alikuwa mmoja wa wageni mashuhuri waliokuwepo…

Read More

Caption: Kasisi Martin Niemoller. Picha ya Nationaal Archief Na Ahmed Rajab SIJUI kwa nini hasa, ingawa nina hakika sababu ninazo, lakini tangu juzi akili yangu imetekwa na ndege na kasisi.  Imekuwa ikivutwa na kuvutiwa na viumbe hivyo. Nimekuwa nikiufikiria ujanja wa ndege na nikiyakumbuka maneno ya Martin Niemöller, kasisi wa Kijerumani aliyepata umaarufu katika zama za udikteta wa Adolf Hitler na siasa zake za Unazi. Siasa hizo za kibaguzi zilisababisha mauaji ya halaiki ya Wayahudi pamoja na wengine ambao Hitler na wafuasi wake wakiamini walikuwa na “damu chafu”, yaani hawakuwa na ile waliyoifikiria…

Read More

Caption. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, akitoa mhadhara kuhusu masuala ya kitaifa na kimataifa wakati alipozungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Tusiime jijini Dar es Salaam mnamo Machi 30, 2015. Picha kutoka Ofisi Binafsi ya Membe. Na Ezekiel Kamwaga   BERNARD Kamillius Membe (69) aliyefariki dunia Mei 9 mwaka huu, alikuwa mtu maarufu nchini Tanzania. Alikuwa maarufu zaidi wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kati ya mwaka 2007-2015; akiweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa pili kushika wadhifa huo kwa muda mrefu zaidi – akizidiwa na Jakaya Kikwete tu aliyehudumu…

Read More

Na Ezekiel Kamwaga WIKI iliyopita, chama cha siasa cha ACT Wazalendo kilitimiza miaka tisa kamili tangu kuanzishwa kwake mnamo Mei mwaka 2014. Ingawa katika muda huo kimepita katika misukosuko mingi, naamini kwamba miaka 10 inayokuja itakuwa muhimu zaidi kwake. Kama ilivyo kwa viumbe hai vingi, chama cha siasa kina maisha ya aina tatu – ya awali wakati kingali kinategemea wazazi na mazingira kuishi, maisha ya kujitegemea na hatua ya tatu ni ile ya ama kufikia malengo au kufa. Kama chama kitavuka hatua ya awali kikiwa salama, uwezo wa kudumu katika hatua ya pili kama chama tawala au cha…

Read More

Na Ezekiel Kamwaga TANGU aingie bungeni kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amekuwa na tabia moja inayomtofautisha na wabunge wengi – kwamba huwa haingii ndani ya viwanja vya Bunge jijini Dodoma kwa kutumia gari yake. Badala yake huacha gari yake nje na kutembea kwa miguu kuingia ndani ya Bunge. Nimewahi kumwuliza wakati fulani kwa nini haingii ndani na gari na jibu lake lilionyesha busara kubwa; “Nataka kutumia dakika chache hizo kusalimiana na watu na kuzungumza na wale nitakaokutana nao njiani. Ukiingia na gari hadi ndani, unakosa…

Read More

Na Ezekiel Kamwaga WIKI hii nimetimiza miaka 20 tangu nianze rasmi kazi ya uandishi wa habari. Katika muda huo nimefanya kazi katika vyombo tofauti vya habari – kuanzia kampuni ya Habari Corporation iliyonipa kazi ningali kijana mdogo, na mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya Tanzania. Nimeamua nitumie makala hii kuwakumbuka waandishi wenzangu niliowahi kufanya nao kazi ambao sasa wametangulia mbele ya haki. Hawa ni watu niliokuwa na uhusiano nao wa aina tofauti; kuanzia marafiki, mabosi, washauri na watu ambao kwa namna moja au nyingine waliongeza kitu katika maisha yangu kama mwanataaluma na mwanadamu. Nimetengeneza gazeti kutoka…

Read More