Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
Author: Ezekiel Kamwaga
Na Ezekiel Kamwaga AKIANDIKA mapitio ya kitabu cha The Age of Revolutions cha Fareed Zakaria kwenye jarida mashuhuri la Foreign Policy Machi mwaka jana, mchambuzi Michael Hirsh, aliandika mstari mmoja ambao umebaki kwenye kumbukumbu zangu; “Kuna kitu kimeikumba dunia hivi sasa na sote bado hatujajua ni kitu gani”. Hayo yalikuwa ni mawazo yangu pia wiki hii baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yaliyompa ushindi Tundu Lissu dhidi ya aliyekuwa akishika wadhifa huo, Freeman Mbowe. Mimi niliamini kwamba hakuna uwezekano wa Lissu kumshinda Mbowe.…
Na Ezekiel Kamwaga UTANGULIZI WAKATI mwaka mpya unapoanza, vyombo vya habari vimekuwa na utamaduni wa kufanya tafakuri kuhusu masuala tofauti yaliyotokea katika mwaka uliokwisha na yapi ya kutarajia katika mwaka mpya. Kwa mara ya kwanza mwaka huu, Gazeti la Dunia linafanya uchambuzi wa kuangalia wanasiasa wa kuangaliwa zaidi katika mwaka 2025. Tumeamua kuchagua wanasiasa kwa sababu kuu mbili; Mosi kwamba huu ni mwaka ambao Tanzania inatarajiwa kufanya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani na pili ni kupunguza idadi ya watu wanaoweza kuingia kwenye orodha hii. Na tumeamua kuandika…
Na Ezekiel Kamwaga MWAKA 2015, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilipata mafanikio makubwa katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania. Kilipata takribani asilimia 40 ya kura zote zilizopigwa – kiwango ambacho kilikuwa hakijawahi kufikiwa na chama chochote cha upinzani katika historia ya taifa letu. Kulikuwa na mambo mawili katika ushindi huo wa CHADEMA. Mosi ilikuwa ni ukweli kuwa kilishinda chini ya mwavuli wa UKAWA na pili kikawa chama cha kwanza cha upinzani kujikuta kina mawaziri wakuu wawili wastaafu ndani ya Kamati Kuu yake. Nyuma ya ushindi ule mkubwa alikuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman…
Picha kwa Hisani ya Gazeti la Citizen la Tanzania Na Ezekiel Kamwaga MARA nyingi ninapofanya uchambuzi kuhusu wanasiasa, huwa ninaamini kuwa kuna wanasiasa wa aina tatu; wanasiasa wa kipekee, wanasiasa wa kitaasisi na wanasiasa wa msimu. Wanasiasa wa kipekee ni wale ambao si wa kawaida. Nazungumzia watu wa aina ya Nelson Mandela wa Afrika Kusini, Kwame Nkrumah wa Ghana, Julius Nyerere wa Tanzania na wengine wa aina hiyohiyo. Kwa sababu za kihistoria na za kimuktadha, nchi nyingi hazizalishi viongozi wengi wa aina hii. Wanasiasa wataasisi ni wale ambao wao hujenga taasisi za kisiasa katika mazingira ambayo…
Na Ezekiel Kamwaga KATIKA uchambuzi wake wa nini kilisababisha Mapinduzi ya Ufaransa ya mwaka 1789, Alexis du Tocqueville aliandika kitu cha tofauti na wengine walioandika kuhusu mapinduzi yale. Alisema mapinduzi yale hayakuwa tukio la mara moja bali ni hitimisho la miaka mingi ya kuharibika kwa mfumo wa utawala wa taifa hilo. Katika andishi lake maarufu la mwaka 1856, L’Ancien Régime et la Révolution (The Old Regime and the French Revolution), Tocqueville alitumia muda mrefu kuisaili jamii ya Wafaransa kiundani kuelekea kwenye mapinduzi. Tukio la hivi karibuni la kutekwa kwa Mwenyekiti wa Ngome ya…
MAELEZO YA PICHA: Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo ya uwili (bilateral) na Rais wa Indonesia, Prabowo Subianto, pembezoni mwa mkutano wa G20 uliofanyika Rio de Janeiro, Brazil, wiki iliyopita. Na Ezekiel Kamwaga MOJAWAPO ya taswira zilizobaki kwenye kumbukumbu zangu kuhusu Mkutano wa Nchi Tajiri Duniani maarufu kwa jina la G20 uliomalizika jijini Rio de Janeiro, Brazil wiki iliyopita, inahusu mkutano ambao Rais Samia Suluhu Hassan alifanya na wahariri wa vyombo vya habari vya Tanzania waliokuwa kwenye msafara wa Rais kwenye tukio hilo. Nakumbuka kumwona Rais Samia akiingia kwenye ukumbi wa mkutano huku akijaribu kusoma maandishi…
Na Ezekiel Kamwaga DAKIKA chache baada ya ndege iliyombeba Rais Samia Suluhu Hassan kupaa angani kwenda Brazil kuhudhuria mkutano aliopewa heshima ya kualikwa wa Nchi Tajiri Duniani wa G20, habari zilianza kusambaa mitandaoni kuhusu kuanguka kwa jengo la biashara katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam. Kwa bahati nzuri, ndani ya ndege hiyo kubwa ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) aina ya Dreamliner maarufu kwa jina la Hapa Kazi Tu, kuna huduma ya internet na abiria tuliokuwa ndani ya ndege hiyo na katika mitandao ya kijamii, tulikuwa tunafuatilia kilichokuwa kinaendelea. Kama mwandishi wa habari…
Na Ezekiel Kamwaga KESHO, Septemba 23, 2024, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepanga kufanya maandamano hapa nchini kupinga vitendo vya utekaji na mauaji vinavyoonekana kukithiri hapa nchini hivi sasa. Mpaka wakati naandika makala haya, ninafahamu kwamba CHADEMA wameamua kesho watafanya maandamano hayo. Na mpaka wakati huu, Polisi hawajatoa taarifa yoyote kuruhusu kufanyika kwa maandamano hayo. Taarifa iliyopo ni kwamba maandamano hayo hayataruhusiwa. Mimi ni mwanafunzi wa siasa za hapa nyumbani na za bara letu la Afrika. Kwa hapa tulipofika sasa, sioni uwezekano wa jambo hili kumalizika kwa amani endapo busara haitatamalaki kutoka upande mmoja au…
Tajiri Elon Musk wa Marekani (kushoto) katika picha na mgombea urais wa chama cha Republican, Donald Trump. Picha kwa hisani ya IBTimesUK Na Ezekiel Kamwaga KWA wafuatiliaji wa siasa za Marekani kuelekea uchaguzi wao wa Novemba mwaka huu, watakuwa wamebaini namna Elon Musk; mmoja wa matajiri wakubwa duniani, anavyomuunga mkono mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump. Kama Musk angekuwa Tanzania, pasi na shaka yoyote angepachikwa jina la Chawa. Kwenye siasa zetu, neno chawa limekuwa likinasibishwa na ufuasi wa mtu kwa wanasiasa au viongozi. Lakini swali ambalo nitajaribu kulijibu kupitia makala haya…
Na Ezekiel Kamwaga SIKU moja majira ya saa tano usiku, nilipokea simu kutoka kwa mwanasiasa mkongwe wa Zanzibar, Juma Duni Haji. Alikuwa ananipigia kwa vile hakupokea wakati alipopigiwa simu kutoka kwangu saa kadhaa nyuma. Nilipoiona tu nilitabasamu maana nilijua kilichotokea. Sikuwa nimempigia mimi isipokuwa binti yangu mwenye umri wa miaka mitatu wakati huo. Kwa sababu ya namna simu yangu nilivyohifadhi majina, jina la Babu Duni lilikuwa miongoni mwa majina ya mwanzo na sijajua kwa nini ilikuwa binti akipiga inapigwa kwa waziri huyo wa zamani. Siku hiyo akaniambia kwa utani tu; “Najua leo kapiga simu mchumba wangu,…
