Author: Ahmed Rajab

Picha: Mmoja wa waandamanaji akifurahia hukumu ya Mahakama ya Haki ya Kimataifa (ICJ) dhidi ya Israel jijini The Hague hivi karibuni. Picha kwa hisani ya Foreign Policy Na Ahmed Rajab ISRAEL haina uso.  Inajaribu kujikaza kisabuni na kujitoa kimasomaso lakini Mahakama ya Kimataifa (ICJ), mjini Hague, Uholanzi, yameiumbua kwa unyama inaoufanya dhidi ya wakaazi wa Gaza. Ijumaa iliyopita, Januari 26, 2024, Mahakama hayo — ambayo ni ya juu kabisa kimataifa — ilitoa uamuzi wake kuhusu mashtaka yaliyowasilishwa na Afrika Kusini. Nchi hiyo iliishitaki Israel kwa kufanya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza. Afrika Kusini iliyataka…

Read More

Rais Joe Biden akiwa na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. Picha ya Shirika la AP Na Ahmed Rajab ZAIDI ya siku mia zimekwishapita tangu majeshi ya Israel yaanze kulitwanga eneo zima la Ukanda wa Gaza, ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi mashambulio yakushangaza dhidi ya Israel yaliyofanywa na Mvuvumko wa Muqawama wa Hamas mnamo Oktoba 7, 2023. Waisraeli 1,200 walikufa na watu 240 wa mataifa kadhaa walishikwa mateka na Hamas. Mashambulio hayo ya Oktoba 7, ambayo Hamas inayaita Gharika ya Al-Aqsa, yalikuwa ya kulipizia kisasi madhila, unyanyasaji, mateso, na mauaji ya Wapalestina  katika Ufukwe wa Magharibi…

Read More

Picha: Rais Donald Trump. Picha kwa hisani ya mtandao wa AP. Na Ahmed Rajab SITOSHANGAA ukinambia hujui “ujutar” ni nini au “jutar” ni nani.  Niliwauliza watu kadhaa wa sehemu mbalimbali za Uswahilini na wapo walionambia hawajawahi kuzisikia kalima hizo mbili. Nimechungulia kwenye makamusi mawili matatu ya Kiswahili humo namo sikuyaona. Hata hivyo, tuko wengi wa mjini Unguja tulioyasikia na tunaoyatumia maneno hayo mawili. Mimi nayakumbuka tangu utotoni mwangu. Nilikulia na kucheza pamoja na watoto wenzangu waliokuwa pia wakizungumza lugha zitokazo Bara Hindi, hasa Kigujarati. Niliweza kuokota maneno ya Kigujarati na kutunga sentensi chache kwa lugha…

Read More

Rais Julius Nyerere akiwa na Henry Kissinger jijini Dar es Salaam mwaka 1976. Picha kwa Hisani ya Cambridge University Press Na Ahmed Rajab DAKTA Henry Kissinger aliyefariki dunia Kent, Connecticut, Marekani, Novemba 29 mwaka huu alikuwa mwingi wa mengi.  Alikuwa msomi wa hali ya juu, gwiji wa diplomasia, mshauri wa siasa za kimataifa na mwanasiasa. Kabla ya kuzivaa siasa, Kissinger alikuwa akisomesha katika Chuo Kikuu cha Harvard, kimoja kati ya vyuo vikuu ‘babu kubwa’ duniani.  Miongoni mwa wanafunzi wake alikuwa kijana kutoka Uganda, Mahmood Mamdani, ambaye sasa ni profesa aliyebobea wa sayansi ya siasa. Uzoefu wa…

Read More

Picha kwa Hisani ya Pars Today Na Ahmed Rajab KISWAHILI chetu hakina neno moja lenye tafsiri ya neno la Kiingereza ‘resistance.’ Lakini lugha za Kiarabu na Kifarsi (Kiajemi), ambazo tumezoea kuazima misamiati yao, zote zinalo neno moja lenye maana ya ‘resistance.’ Na lugha zote hizo mbili zinalitumia neno hilo hilo moja lililoanzia kwenye Kiarabu: ‘muqawama.’ Baadhi ya Waswahili wenye uzoefu wa mojawapo wa lugha hizo, ama Kiarabu au Kifarsi, nao pia huliangukia neno ‘muqawama’ linaposibu kutumika. Kwa mfano, Idhaa ya Kiswahili ya Radio Tehran hulitumia neno hilo kwenye matangazo yake na pia katika mtandao wake wa Pars Today. …

Read More

Picha: Nakala ya kitabu kilichoandikwa na Profesa Aili Mari Tripp kuhusu maisha ya Joan Wicken na uhusiano wake na Mwalimu Nyerere. Kitabu hicho kimechapwa na kampuni ya Mkuki na Nyota Na Ahmed Rajab KWA zaidi ya miaka 40, kila alasiri baada ya saa za kazi, Bi Joan Wicken alikuwa akikimbilia Msasani, Dar es Salaam, nyumbani kwa Mwalimu Julius Nyerere. Ulikuwa muda wao wa faragha.  Wakizungumza kwa saa nzima kuanzia saa kumi na moja hadi jua lilipokuwa likizama. Kama palikuwa na vinywaji, basi Wicken akipiga pombe kali ya Whiskey, aliyokuwa akiipenda, na Nyerere akibugia mvinyo wa Kireno wa Mateus…

Read More

  Na Ahmed Rajab   UJUMBE wa simu ulipoingia asubuhi ya Ijumaa iliyopita, ulikuwa na maneno machache: “Ndugu yetu ameshatangulia mbele ya Haq leo saa moja na dakika arobaini na tano kwa saa za hapa. Tunangoja daktari aje kumtizama mara ya mwisho.” Aliyeleta ujumbe alikuwa Hamed Hilal, mmoja wa makomredi wa chama cha zamani cha Umma Party cha Zanzibar, kilichokuwa kikifuata itikadi ya Umarx.  Huyo “ndugu” yetu aliyetutoka alikuwa komredi mwenzetu, Hashil Seif Hashil, aliyefariki saa hizo jijini Copenhagen, Denmark. Ujumbe wa Hamed ulitanguliwa na aya ya Qur’ani isemayo, “Inna liLlahi wa inna ilayhi rajiun” (Hakika sisi ni…

Read More

Maelezo ya Picha. Aliyekuwa Kiongozi wa Wapalestina, Yasser Arafat (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa zamani wa Comoro, Ahmed Abdallah (kushoto) na aliyekuwa Mufti wa Comoro Sayyid Muhammad Abdulrahman (kulia), wakati alipotembelea taifa hilo kwenye miaka ya nyuma. Na Ahmed Rajab ‘Je, Israeli ni dola la ubaguzi wa kikabila?’ Nilimuuliza mwandishi habari maarufu wa Israeli Gideon Spiro kwenye mkahawa wa Bookworm Café jijini Tel Aviv, Mei 2009. Bookworm ni duka la vitabu lakini lina mkahawa na ni mahali ambapo Waisraeli wa mrengo wa kushoto hukutana. Sijui kwa nini nilimuuliza Spiro swali hilo kwani nikijua kwamba…

Read More

Picha: Kiongozi wa zamani wa Wapalestina, Yasser Arafat, kwenye picha na Mwalimu Nyerere. Na Ezekiel Kamwaga Katika moja ya hotuba zake maarufu za zamani, Baba wa Taifa la Zambia, Dk. Kenneth Kaunda, alipata kuelezea uhusiano baina ya taifa lake na Tanzania kuwa sawa na ule wa pacha walioungana. Hakuna kilichokuwa kinaeleza uhusiano huo kama uhusiano baina yake na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Wawili hawa walipendana kiasi kwamba Kaunda aliamua kumpa mmoja wa watoto zake jina la Kambarage – ambalo ni moja ya majina ya Mwalimu Nyerere. Na hata wakati alipokuwa akipita katika wakati mgumu kwenye utawala wa mbadala…

Read More

Na Ahmed Rajab NILIPOWASILI Gaza kwa mara ya kwanza Mei 2009 nilikuwa na hamu kubwa ya kukutana na Ismail Haniyeh, kiongozi wa Hamas (ufupisho wa Harakah al-Muqawamah al-Islamiyyah) na aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Palestina.  Hamas ni chama cha kisiasa chenye muelekeo wa Kiislamu; wafuasi wake wanafuata madhehebu ya Sunni. Chama hicho kimekuwa kikiliendesha eneo la Gaza tangu 2007, mwaka mmoja baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa Bunge la Palestina.  Katika uchaguzi huo Hamas kilikibwaga chama cha Fatah, chama kikubwa cha Wapalestina kinachoongozwa na Mahmoud Abbas. Hamas si shetani wa Fatah. Wala si shetani wa Israel.…

Read More