Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
Author: Ahmed Rajab
Mtungaji: Mohammed Ghassani Wachapishaji: Zaima Publishers Uhakiki na Ahmed Rajab KITABU hiki, kilichozinduliwa Oktoba 26, mwaka 2024 kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha SOAS, London, ni cha aina ya pekee. Hakina mfanowe katika fasihi ya Kiswahili — si ya kale, si ya kisasa. Ni vitabu viwili ndani ya kimoja. Kila kitabu kati yavyo kikiwa na uzito wake na nyuzi zenye kuviungaisha — kama si kwa maudhui yao basi kwa hisia zao au vichocheo vya hisia vinavyoyafanya maudhui yao yawe mamoja au yenye kuhusiana. Kila kitabu kati ya hivyo viwili ni mkusanyiko. Cha kwanza, “Mbegu za Tikiti,” ni…
Picha. Salum Badar Na Ahmed Rajab SALUM Badar aliyefariki dunia mjini Malmo, Kusini mwa Sweden, Agosti 13, 2024, akiwa na umri wa miaka 86 alikuwa miongoni mwa Wazanzibari washupavu waliochangia katika harakati za ukombozi bila ya kujigamba au kutambulika au hata kujulikana. Katika siasa za Zanzibar, Salum Badar alikuwa wa mrengo wa kushoto. Akimuunga mkono Abdulrahman Babu aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Umma Party, kilichokuwa kikifuata falsafa ya Umarx. Utiifu wake kwa Babu haukuyumba hata siku moja na alikuwa mfano wa mtu wa tabaka la juu la kimaisha aliyetetea, kwa hali na mali, maslahi ya walio…
Pichani: Ismail Haniyey, aliyekuwa Kiongozi wa Kisiasa wa Chama cha Hamas cha Palestina. Picha kwa hisani ya Getty Image Na Ahmed Rajab WATU wengi wanaposikia mvuvumko wa Hamas ukitajwa, sura ya mwanzo inayowajia ni ya Ismail Haniyeh, aliyekuwa kiongozi wa kisiasa wa chama hicho na aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Palestina baada ya chama chake kushinda uchaguzi mkuu wa Bunge la Palestina mwaka 2006. Sura za vigogo wengine wa Hamas, kwa mfano, kiongozi wake aliye Gaza, Yahya Sinwar au kaimu wake, Khalil al-Hayya, au za makamanda wa kijeshi wa kundi hilo, kama vile Mohamed Dief…
Na Ahmed Rajab HUU ni wakati muhimu na mgumu kwa Kenya. Taifa hilo linawaka moto na siasa zake zimefikia patamu. Rais William Ruto ambaye wiki chache tu zilizopita alionekana kuwa imara hivi sasa ni wazi kwamba amedhoofika. Wapinzani wake waliomiminika barabarani wamelivua guo la woga na wamekuwa na ujasiri wa kutamka wazi kwamba lazima aondoke madarakani. Kuna hoja ya maana kwa nini Ruto anapaswa ajiuzulu na aitishe uchaguzi mkuu mwingine. Ruto amejitia kitanzi kwa kuukataa muswada wake wa Fedha uliokuwa na lengo la kupandisha kodi. Pamoja na kuukataa muswada huo, polisi wake wanatuhumiwa kuwaua waandamanaji chungu nzima.…
KARATA za kisiasa anazozicheza William Ruto, Rais wa Kenya, katika jukwaa la kimataifa zinamfanya aonekane kuwa ama ni mwerevu au ni fala. Kuna wasemao kwamba hana uwerevu wowote lakini si mjinga wala zuzu kwani anajua akifanyacho — amejitolea kuitumikia Marekani na kuwa askari wake katika ukanda wa Afrika Mashariki na katika nchi zinazoendelea, kwa jumla. Kwa ufupi, wanasema kuwa yeye ni kibaraka mwenye kucheza ngoma ipigwayo na Marekani. Tunaifanya tathmini hii ya haraka haraka wakati ambapo Ruto amejitolea kupeleka askari wa Kenya kwenda kutuliza hali tete ya usalama huko Haiti, nchi iliyo takriban kilometa 12, 300 kutoka Kenya,…
Na Ahmed Rajab UHUSIANO baina ya Tanzania na Comoro unatazamiwa kupaa na kukua baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumteua Saidi Yakubu kuwa balozi mpya wa nchi yake visiwani Comoro. Yakubu aliyehitimu shahada ya sheria nchini Uingereza kabla ya kurudi Tanzania na kufanya kazi bungeni na baadaye kuwa katibu mkuu katika wizara ya utamaduni, sanaa na michezo, anasifika kwa utendaji kazi wake. Waliowahi kufanya kazi naye wameliambia Gazeti La Dunia kuwa Yakubu si mtu aliyezubaazubaa, wa kumangamanga, kama wasemavyo vijana siku hizi. Ni mtu mahiri, mwenye kujiandaa kabla ya kupambana na jukumu lolote lililo mbele yake. Si…
Na Ahmed Rajab KUTIMU miaka 60 ya Muungano wa Tanzania mnamo 26 Aprili, 2024, kumezidi kuwasisimua na kuwatia jazba baadhi ya waumini wa Umajumui wa Afrika. Mhemuko wao umewafanya wausukume na wajaribu kuufikisha mbinguni Muungano huo. Wanauelezea kuwa ni mfano thabiti wa umoja halisi wa Afrika. Mashabiki hao wa Muungano wanasisitiza kwamba lazima Muungano huo wa Tanganyika na Zanzibar uangaliwe kwa mtazamo mpana. Wanahoji kwamba fahari na uzito wake wapaswa kuzingatiwa katika muktadha wa historia ya Afrika na mafanikio ya Waafrika katika kupambana na kuushinda ukoloni, ubeberu na itikadi za kibaguzi. Hayo ni maneno…
Na Ahmed Rajab Sura ya nje ya kitabu cha Mtazamo wa Kifikra wa “Sauti ya Dhiki” ya Abdilatif Abdalla. Mashairi yamefasiriwa kwa Kiingereza na Ken Walibora Waliaula na kitabu kizima kimehaririwa na Annmarie Drury. Kitabu hicho chenye kurasa 344 kimechapishwa na University of Michigan Press na Afrika kimechapishwa na Mkuki na Nyota Publishers, Dar es Salaam, Tanzania. KITABU hichi tunachokihakiki kimekusanya mengi yenye kukifanya kiwe tunu kwa wasomaji wa aina mbalimbali. Tena ni cha kihistoria kwa sababu ni kitabu cha kwanza chenye tafsiri ya Kiingereza ya diwani nzima ya “Sauti ya Dhiki”, mkusanyiko wa mashairi uliompatia umaarufu mkubwa…
Na Ahmed Rajab MIAKA kadhaa iliyopita katika siku kama hizi za mfungo wa Ramadhani niliwahi kuandika makala katika gazeti la Raia Mwema ambamo nililalama jinsi aina kwa aina ya mapishi asilia ya Kiswahili yalivyotoweka Zanzibar baada ya Mapinduzi ya 1964. Nilijawa na furaha nilipoona kwamba makala hayo yaliwachochea wengine kuendeleza na kuandika katika mitandao ya kijamii kuhusu mada hiyo. Makala yangu hayajakusudia kuvitaja vyakula vya Zanzibar nzima vilivyoadimika au kupotea kabisa. Nisingaliweza. Nilijikita katika sehemu tu ya Mjini, Unguja, nilikozaliwa na kukulia. Kumbukumbu zangu zilinipeleka kwenye mitaa ya Vuga, Mkunazini, Kajificheni, Shangani na Baghani. …
TAABINI Ali Hassan Mwinyi “Mzee Rukhsa”: (Mei 8,1925 – Februari 29, 2024) Mtu wa watu aliyependwa na masharifu ALHAJI Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki dunia Dar es Salaam, Alhamisi iliyopita, siku 70 kabla ya kutimia miaka 99, aliushangaza ulimwengu alipoibuka kuwa Rais wa tatu wa Zanzibar 1984. Mwinyi aliushangaza tena ulimwengu miezi kadhaa baadaye alipochomoza kuwa Rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hadi sasa ni yeye tu aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar na wa Tanzania. Alipoushika urais wa Zanzibar machepe wa mitaani wakisema kwamba urais huo ulimjia kama “riziki dudu”. Hakuulalia, hakuuamkia. Kabla ya hapo huko huko Zanzibar,…
