Author: Ahmed Rajab

Picha: Maalim Seif Sharif Hamad na Dk. Salim Ahmed wakizungumza wakati Salim akiwa Mjumbe wa Kamati ya Bunge la Katiba. Na Ahmed Rajab NILIWAHI kuandika kuhusu mazungumzo yangu na Mwalimu Julius Nyerere alasiri ya tarehe 5 Desemba, 1994, chumbani kwake katika hoteli ya Intercontinental, jijini Nairobi. Ilikuwa miezi saba kabla ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kumchagua mgombea wake katika uchaguzi wa urais wa mwaka 1995. Mwalimu aliniuliza watu wanasemaje kuhusu mchakato huo, nami nikamjibu: “Wanasema una mgombea wako.” “Nani?” “Salim,” nikamjibu, nikimkusudia Dkt. Salim Ahmed Salim. “Kwa nini?” Mwalimu aliendelea kunisaili. “Kwa sababu…

Read More

Picha: Mwandishi wa makala haya, Ahmed Rajab (kushoto), akiwa na mwandishi mwenzake wa Tanzania, Salim Kikeke, wakiwa na tuzo zao zilizoenzi mchango wao katika kukuza lugha ya Kiswahili. Tukio hilo lilifanyika London, Uingereza, hivi karibuni.   Na Ahmed Rajab DUH! Ningefedheheka nikashika adabu yangu. Na wanawake ndio wangeliniponza kwani mti huponzwa na tundale. Sijui uso wangu ningeutundika wapi. Safari moja nikiwa ninatembea Tindouf, mji wa jangwani Magharibi mwa Algeria, niliwaona waandishi wa habari wa kimataifa wakiwazunguka viongozi wawili wa chama cha Polisario chenye kupigania ukombozi wa nchi hiyo kutoka ukoloni wa Morocco. Viongozi hao, Bashir na Mouloud,…

Read More

Picha:Ali Muhsin Barwani (kushoto), Kwame Nkrumah na Julius Nyerere (wa pili kulia), Accra, 1958. Picha kwa hisani ya Ahmed Rajab Na Ahmed Rajab WIKI mbili zilizopita niliandika kuhusu mazungumzo waliyokuwa nayo viongozi wawili wa kizalendo wa Kiafrika jijini Accra, Machi 1958. Viongozi wenyewe walikuwa Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Ali Muhsin Barwani. Nyerere alikuwa rais wa Tanganyika African Union (TANU), chama kilichokuwa kikipigania uhuru wa Tanganyika, na Barwani alikuwa kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (ZNP, au Hizbu), chama pekee kilichokuwa kikipigania uhuru wa Zanzibar kwa wakati huo. Nilieleza kwamba walipokuwa wakizungumza katika hoteli ya Aveneda, waliambizana shida zao.…

Read More

Picha. Mwandishi wa makala haya, Ahmed Rajab (kushoto), akizungumza na Rais mstaafu wa Nigeria, Ibrahim Babangida, nyumbani kwake wakati wa mahojiano yaliyofanyika nyumbani kwa kiongozi huyo nchini Nigeria. Na Ahmed Rajab KAMA kuna mtawala wa kijeshi aliyewaweza Wanigeria basi alikuwa Ibrahim Badamasi Babangida (IBB) au “Maradona”, kwa umaarufu wake wa mitaani. Si bure kwamba alibandikwa lakabu hiyo ya jina la mchezaji soka maarufu wa zamani wa Argentina. Sidhani kuwa kuna atakayesahau namna IBB alivyokuwa akicheza katika medani ya siasa za Nigeria, akiwapiga chenga Wanigeria wenzake, na hususan wanasiasa kwa miaka minane aliyokuwa madarakani (Agosti 27, 1985…

Read More

Picha: Rais Bola Ahmed Tinubu wa Nigeria. Picha kwa Hisani ya mtandao wa Business NG.   Na Ahmed Rajab SIKU zinaingia na siku zinatoka lakini Afrika Magharibi haziingii tena kwa vishindo.  Hatuyasikii magoma yakipigwa kunadi vita.  Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi (Ecowas) na mwenyekiti wake wa sasa, Rais Bola Ahmed Tinubu wa Nigeria, wanaonesha kama wamekwama. Tinubu na Ecowas wanashikilia kuwa wapinduzi wa Niger wamrejeshe madarakani Rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum lakini vitisho vyao kwa sasa ni sawa na nguvu za povu.  Rais Alassane Ouattara wa Côte d’Ivoire ndiye aliyebeba bendera ya kutaka ‘demokrasia’ irejeshwe Niger. Ouattara…

Read More

Picha: Viongozi wa kundi la askari waliopindua serikali ya Rais Mohamed Bazoum nchini Niger. Picha ya Al Jazeera Na Ahmed Rajab WIKI imepita kama upepo tangu Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi (Ecowas) itangaze kuwa inawapa wapinduzi wa kijeshi wa Niger muda huo wa wiki moja wamrejeshe madarakani Rais waliyempindua, Mohamed Bazoum, na wayazime mapinduzi yao. Ecowas ikatoa vitisho kwamba lau wapinduzi wasipoyatimiza hayo watakiona cha mtema kuni: majeshi kutoka nchi za Ecowas yataivamia Niger kuyazima kwa nguvu mapinduzi hayo na wakati huohuo Niger ikawekewa vikwazo kadhaa. Kwa miezi sasa, picha, kama wasemavyo vijana mitaani zilikuwa…

Read More

Picha: Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume (kushoto), katika mazungumzo na Abdulrahman Babu Na Ahmed Rajab SIKU ilipotangazwa kwamba Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitaungana, Abdulrahman Mohamed Babu aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na biashara za nje wa Zanzibar, hakuwako visiwani.  Alikuwa Jakarta, Indonesia, alikokwenda kutafuta masoko ya karafuu za Zanzibar, zao lililokuwa likiipatia Zanzibar pato lake kubwa la fedha za kigeni. Indonesia ilikuwa mshitiri mkuu wa karafuu, ambazo ikizitumia kutengenezea sigara, dawa ya meno na viungo vya mapishi. Kwa vile wakati huo Babu alikuwa Jakarta, hakuhudhuria pia kikao cha Baraza la Mapinduzi…

Read More

Picha: Shihabuddin Chiraghdin (kushoto) na Mohamed Hassan Abdulaziz (Kulia). Picha kwa Hisani ya Wanafamilia.  Na Ahmed Rajab PROFESA Mohamed Hassan Abdulaziz aliyefariki dunia jijini Nairobi asubuhi ya tarehe 10 Julai akiwa na umri wa miaka 91 alikuwa gwiji wa isimu, Kiswahili na Kiarabu. Zaidi ya hayo alikuwa msomi wa wasomi wenye kuhusika na mambo ya lugha na alikuwa mwalimu wa waalimu wa fani hiyo. Akiheshimika duniani kote katika duru za wanaisimu. Kwa bahati mbaya si wengi waliokuwa wakimjua kwao Kenya au hata Uswahilini kote licha ya kwamba yeye, mzalia wa Mombasa, na Profesa Farouk Topan, mzalia wa…

Read More

Mwandishi wa makala haya, Ahmed Rajab, akizungumza kwenye Baraza la House of Lords jijini London Julai 5, 2023. Hapa alikuwa akitoa mada kuhusu Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili. Picha kwa Hisani ya Karam Bharij.  Na Ahmed Rajab JUMATANO ya wiki iliyopita, nilimpigia simu mhariri wetu wa Gazeti la Dunia nikamwambia kwa ukali kwamba lau ningelikuwa karibu naye ningechukua bakora nikamchapa.  Namna mhashamu huyu alivyonijibu kulinifanya nimuonee huruma kidogo kwa sababu alinijibu kwa unyonge na mshangao. “Kwani nimefanya nini?” aliniuliza. Nikamueleza kwamba aliandika kwenye Twitter neno “RUKSA”, tena kwa herufi kubwa, neno ambalo halimo…

Read More

 Mwandishi wa makala haya, Ahmed Rajab, akiwa kwenye handaki eneo la Jamba, Angola, ilikokuwa kambi ya kijeshi ya kundi la waasi la UNITA. Kunradhi kwa mwonekano wa picha. Mazingira ya ndani ya handaki yamefinya mwonekano. Picha kwa hisani ya Ahmed Rajab.    Na Ahmed Rajab ILIKUWA alasiri Januari 1991 na nilikuwa nimejikalia kivivu ofisini mwangu London kwenye jarida la Africa Analysis, nililokuwa nikilihariri.  Mara ikalia simu ambayo hatimaye ilinifikisha kwa Jonas Savimbi na jeshi lake la waasi katika pori la Angola. Aliyepiga simu alijitambulisha kuwa ni Isaias Samakuva, aliyekuwa mwakilishi wa London wa chama cha União Nacional para…

Read More