Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
Author: Ahmed Rajab
Picha: Prighozin na vikosi vya Wagner barani Afrika. Picha ya jarida la Foreign Affairs Na Ahmed Rajab PAKIZUKA zahama kama zile za Jumamosi iliyopita zilizozushwa na Yevgeny Prigozhin, kiongozi wa Kundi la Wagner, si uzuri mtu kukurukupwa na kuanza kusema asiyoyajua. Ni kheri auzuie mdomo wake au kalamu yake mpaka vumbi litapotulia. Nasema hivi kwa sababu aghalabu pakizuka ghafla sokomoko kama hilo tuyaonayo siyo hali halisi ya mambo yalivyo. Kwa mfano, kuna uwezekano kwamba sakata lote hili ni kiini macho cha Vladimir Putin, Rais wa Urussi, la kuwawekea mtego NATO pamoja na maadui zake waliojificha ndani ya…
Picha: Putin na Rasputin. Picha ya Washington Times Na Ezekiel Kamwaga TUKIO la mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo vikosi vya majeshi ya mamluki wa Wagner Group vinavyoongozwa na Yevgeny Prigozhin kusogea hadi takribani kilometa 400 kutoka Mji Mkuu wa Urussi katika kilichoonekana kama mwanzo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, liliwashangaza wengi. Inajulikana kwamba Prigozhin ni swahiba wa muda mrefu wa Rais Vladimir Putin na mambo yote yanayofanywa naye na mamluki wake yana baraka za mtawala huyo wa Urusi kwa takribani miongo mitatu. Swali ambalo wengi walikuwa wakijiuliza ni kwamba nini kimesababisha wawili hao kukorofishana kiasi cha…
Picha: Baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika wanaoshiriki katika juhudi za upatanishi wa amani katika Vita ya Ukraine, wakiwa na Rais wa taifa hilo, Volodymyr Zelensky jijini Kiev wiki iliyopita. Viongozi wanaoonekana pichani ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Azali Assoumane, kulia kwa rais huyo. Wengine kutoka kushoto ni marais Macky Sall wa Senegal, Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na Hakainde Hichilema wa Zambia. Picha kwa Hisani ya Al Jazeera Na Ahmed Rajab KUNA walioishangilia na kuna walioikebehi taarifa ya kwamba nchi za Kiafrika zinapeleka ujumbe Ukraine na Urussi kujaribu kuzipatanisha nchi hizo. Hisia zote hizo…
Caption: Viongozi wa juu wa CHADEMA katika picha ya pamoja wakati wakitangaza Operesheni Ukuta mnamo Julai mwaka 2016. Ukuta ndiyo ilikuwa jitihada za awali kabisa za vyama vya upinzani kupinga zilizoanza kuonekana kama dalili za awali za udikteta kwenye siku za mwanzo za utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano. BARAZANI KWA RAJAB Na Ahmed Rajab NCHINI Haiti watoto wadogo walio watundu, wakitaka kutishwa, huambiwa kwamba wataitiwa “Tonton macoute” (Mjomba gunia). Huambiwa kwamba mjomba huyo atawatia kwenye gunia ende akawale kwa chakula cha istiftahi, cha kufungulia kinywa. Utukutu huyayuka mara tu watoto hao wanapotajiwa Tonton macoute. Huliogopa zimwi wasilolijua…
Picha: Badawi Qullatein Na Ahmed Rajab BADAWI Qullatein aliyefariki dunia Makkah, Saudi Arabia, asubuhi ya Oktoba 31, 2011 akiwa na umri wa miaka 81 alikuwa ni mtu wa vipaji vingi: mpigania haki za wafanya kazi, mwanamapinduzi, mhariri wa magazeti na mcha Mungu. Alikuwa mtu wa dhihaka nyingi na maskhara mengi ingawa baadhi ya nyakati akipandisha hamaki. Na ulipomwambia mbona umekasirika, akijibu: ‘Unanikasirisha, kwa nini nisikasirike? Sifa nyingine ya Badawi ilikuwa ya ukaidi. Hata hivyo, atakumbukwa zaidi kwa jinsi alivyoutumia ujana wake kuwatetea walala hoi na kupigania haki zao. Yeye ni mfano mzuri wa mtu wa tabaka la wenye kujiweza…
BARAZANI KWA RAJAB Na Ahmed Rajab MARA ya mwanzo kabisa kukutana na Mwalimu Julius Nyerere, uso na macho, ilikuwa 1968 jijini London ndani ya ukumbi mmoja wa hoteli iitwayo Hyde Park. Hoteli hiyo iko mkabala wa uwanja wa Hyde Park na iko mwendo wa dakika chache kutoka Hertford Street ulipokuwako siku hizo ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza. Sikumbuki iwapo Nyerere alikuwa akipita njia London kuelekea kwingine au iwapo alikuja kwa ziara mahsusi nchini Uingereza. Wakati huo Nyerere alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ulikuwa na umri mdogo wa miaka minne. Ukumbi wa mkutano…
Na Ahmed Rajab SIKU hasa siikumbuki. Lakini mwezi na mwaka naukumbuka. Na siku zenyewe kwa jumla ninazikumbuka. Zilikuwa siku za Morogoro Jazz Band na Mbaraka Mwinshehe. Simba Wanyika hawakuwa wakinguruma, walikuwa bado kuzaliwa. Hiyo siku mahsusi nisiyoikumbuka ni siku Rais Julius Nyerere wa Tanzania alipowaita mawaziri wake akawaeleza jambo ambalo hadi leo, miaka 55 baadaye, bado linazusha utata katika kumtathmini Nyerere aliyekuwa akijinata kuwa alijitolea kupigana bara la Afrika liungane kisiasa na kiuchumi. Sina hakika kama siku hiyo ilikuwa Aprili 13, 1968 au siku moja au hata mbili kabla ya hapo. Jengine nisilo na hakika nalo ni iwapo Nyerere alipowaita…
Na Ahmed Rajab WAINGEREZA walipomtia kitanzi na kumnyonga Dedan Kimathi, mimi nilikuwa mdogo — sikuwa nimebalehe kimaumbile wala kisiasa. Wala siku hizo sikujua Dedan Kimathi alikuwa nani. Hata kumsikia sikumsikia. Kimathi alinyongwa asubuhi ya Februari 18, 1957 katika gereza la Kamiti karibu na Nairobi. Kamiti ni gereza lenye ulinzi mkali tangu zama hizo za ukoloni hadi leo. Ni gereza lenye mazingira machafu, lenye ukosefu wa maji na hata nafasi ya kutosha kwa idadi kubwa ya wafungwa wake. Wafungwa gerezani humo huteswa kinyama. Na wenyewe kwa wenyewe hufanyiana mabaya. Baadhi ya wafungwa wana tabia ya “kuwasaka” na kuwalawiti kwa nguvu wafungwa…
