Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
Author: Ezekiel Kamwaga
Na Ezekiel Kamwaga KATIKA kipindi cha takribani miaka 60 ya nchi yetu – na pengine duniani kwa ujumla, P mbili; Perfomance and Politics (Siasa na Utendaji), zimeamua uwepo wa waziri au mawaziri kwenye Baraza la Mawaziri. Rais anaweza kumbadili au kubadili mawaziri kwa sababu ya utendaji wao mbovu au kwa sababu za kisiasa. Wakati wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete – kwa mfano, kuna mawaziri mpaka waliitwa majina ya “mizigo” kwa sababu ya utendaji wao usioridhisha na waliondolewa kwenye baraza. Wakati huohuo wa Kikwete, alilazimika kukubali kujiuzulu kwa Edward Lowassa kama Waziri Mkuu ingawa wakati…
Mwonekano wa majengo pacha ya Tanzania Tower mara yatakapokamilika Na Ezekiel Kamwaga MAPEMA mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Nje, January Makamba, alipokea simu kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Serikali ya Nigeria kuhusu suala la kiwanja ambacho Tanzania ilipewa katika eneo zuri la Lagos takribani miaka 34 iliyopita lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika. January aliulizwa kama Tanzania bado inahitaji eneo lile au serikali ya Nigeria ilipangie matumizi mengine. Itoshe tu kusema kwamba mara baada ya mazungumzo yao, Nigeria ilikubali kuliacha jengo lile kwa matumizi ya Tanzania kama ilivyokuwa makubaliano ya awali. Jambo hilo…
Picha kwa hisani ya tovuti ya Al Jazeera Na Ezekiel Kamwaga NILIPIGA kura kwa mara ya kwanza mwaka 2000 na jambo moja nililolishuhudia wakati ule halijatoka kichwani kwangu hadi leo. Wakati naingia kupiga kura, nilikutana na wasimamizi wawili waliokuwa na mazungumzo ya ajabu kidogo. Mmoja alisema; “Eti hawa wapinzani wanataka kuitoa CCM madarakani. Hii tusikubali, watatuletea vita”. Wakati ule, ingawa nilikuwa mwanafunzi wa kidato cha tano, sikuwaonea haya, niliwaambia kwamba hakuna vita yoyote itakayoletwa na upinzani. Walipigwa na butwaa. Naamini hawakutegemea mwanafunzi kuwaambia maneno yale. Nimeyakumbuka maneno yale wakati nikimsoma mmoja wa…
Picha: Ramani ya Afrika ikionyesha idadi ya kambi za kijeshi za mataifa makubwa ndani ya bara hilo. Hizi ni takwimu za mtandao wa REDDIT. Na Ezekiel Kamwaga KATIKA moja ya mahojiano muhimu zaidi niliyowahi kufanya kama mwana habari, nakumbuka niliyofanya wakati wa awamu ya kwanza ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete. Nilipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Kulikuwa na minong’ono kuwa Marekani ilikuwa na mpango wa kufanya Tanzania kuwa Makao Makuu ya Kamandi yake ya Kijeshi Afrika (AFRICOM). Afande yule, alinieleza kuwa…
Picha kwa hisani ya blogu ya Full Shangwe Na Ezekiel Kamwaga MEI 23 mwaka huu, watu 13 walipoteza maisha baada ya kuungua na mvuke wa moto uliotokea katika kiwanda cha sukari cha Mtibwa kilichopo mkoani Morogoro. Mara baada ya ajali kutokea, tuliambiwa kwamba ripoti ya awali kuhusu nini hasa kilitokea ingetolewa kwa umma wakati uchunguzi zaidi ukiendelea. Imepita zaidi ya wiki moja sasa na hakuna ripoti ya uchunguzi wa tukio hilo – walau ya awali, ambayo imetolewa. Na kama hisia zangu za kiuandishi zinanielekeza vizuri, hakuna hamu kwa wahusika kuzungumza chochote kutokana na ajali hiyo. …
Na Ezekiel Kamwaga WIKI iliyopita nilikuwa nchini China kwenye ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, kufuatia mwaliko wa mwenzake wa China, Wang Yi. Ilisadifu kwamba ziara hiyo iliendana na maadhimisho ya miaka 60 ya nchi hizi mbili lakini pia miaka 75 ya uhusiano baina ya China na Russia. January na Putin walipishana kwa takribani siku mbili – Putin akiandaliwa dhifa na mwenyeji wake, Rais Xi Jin Ping huku January akiandaliwa na mwenyeji wake Wang – na katika matukio yote mawili; ujumbe ulikuwa ni namna ya kutengeneza mfumo mpya…
Na Ezekiel Kamwaga MWAKA jana, marais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Xi Jin Ping wa China walifanya mabadiliko katika mabaraza yao ya mawaziri na kuwapa nafasi wanasiasa wawili ambao ndiyo wasaidizi wao wakuu kwenye masuala ya diplomasia na uhusiano wa kimataifa. Julai mwaka 2023, Rais Xi alimteua mwanadiplomasia mbobezi, Wang Yi, kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa taifa hilo. Miezi miwili baadaye, Rais Samia akamteua January Makamba kushika nafasi hiyohiyo kwa upande wa Tanzania. Wawili hawa wanapishana kiumri kwa takribani miaka 20 January akiwa na umri wa miaka 50 wakati mwenzake huyo akiwa na umri…
Na Ezekiel Kamwaga MAPEMA kabisa, ni muhimu nikaweka wazi kwa nini naandika uchambuzi huu. Kwanza Msumbiji ni rafiki wa damu wa Tanzania, pili kwenye mpaka wetu nao kuna tishio la kiusalama na tatu tunapakana katika eneo ambako huenda nchi yetu ikafanya mradi mkubwa zaidi wa uwekezaji kwenye historia yake – wa LNG. Ni nchi chache sana zina uhusiano zinatuhusu kidamu, kiusalama na kiuchumi kwa kiasi hiki. Kwa nini Msumbiji ni ndugu zetu wa damu? Kwanza, damu ya mwasisi wa chama tawala cha FRELIMO kilichopambania uhuru wa Msumbiji kwa damu, Eduardo Chivambo Mondlane, ilimwagika katika ardhi yetu baada…
Na Ezekiel Kamwaga KATIKA filamu maarufu ya Clash of the Titans ya mwaka 2010, Liam Neeson – akiigiza kama mungu wa hekaya za Kigiriki Zeus, alitamka maneno “Release the Kraken”. Kraken ni lidubwana lisilo na huruma ambalo Zeus aliagiza lifungiwe baharini, chini ya ulinzi wa Poseidon – mtawala wa baharini kwenye hekaya hizohizo, ili asidhuru wanadamu. Zeus – kwa kutimiza matakwa ya mdogo wake, Hades, aliamua Kraken afunguliwe kufanya uharibu kwa vile wanadamu walikuwa wamekosea miungu hiyo. Ni stori ndefu lakini mwishowe Kraken hakufanikiwa kuumiza wanadamu kwa sababu alizuiwa na mwanadamu aliyekuwa na sifa ya kuwa nusu mungu na…
Na Ezekiel Kamwaga NI kazi ngumu kubashiri uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, kwenye nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho. Ukiangalia waliochukua nafasi hiyo kabla, huwezi kutunga uzi au shanga kuunganisha matukio. Hakuna sababu ya waziwazi ya kusema kwa nini alimpa nafasi kwanza Shaka Hamdu Shaka. Aliyemfuatia Shaka, Sofia Mjema, hana sifa za kipekee kulinganisha na wana CCM wengine waliopo Tanzania. Mbadala wa Mjema, Paul Makonda, hakuwa na lolote la kumfananisha na watangulizi wake hao wawili zaidi ya kuwa wanachama wa chama tawala. Hii maana yake ni kwamba mwana…
