Author: Ezekiel Kamwaga

Na Ezekiel Kamwaga KUNA uhusiano wowote kati ya siasa na majengo? Kuna uhusiano wowote baina ya viongozi na matukio ya kujenga au kubomoa vitu? Jibu langu ni ndiyo na makala yangu hii itaeleza juu ya mifano na namna kujenga au kubomoa kunavyoweza kumjenga mwanasiasa au utawala mbele ya wananchi wake. Ninaandika makala haya kwa sababu wiki hii nimebaini kuwa kuna wanasiasa na viongozi wetu mashuhuri ambao kwa bahati mbaya somo kuhusu hili halijawaingia  – na pengine halijawahi kuwa vichwani mwao. Na nadhani, tatizo kubwa la wanasiasa wa mrengo wa kiliberali duniani hivi sasa ni kwamba hawajapata somo…

Read More

Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Karume (kushoto) katika mojawapo ya mazungumzo ya faragha aliyowahi kuyafanya na aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, marehemu Seif Shariff Hamad, kisiwani Unguja. Picha kwa hisani ya gazeti la Mwananchi. Na Ezekiel Kamwaga BAADA ya maneno ya kujibizana baina ya viongozi wa vyama viwili vikuu vya siasa visiwani Zanzibar – Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT Wazalendo, kuhusu mwenendo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUKI), hatimaye Rais mstaafu, Amani Karume, ametoa kauli yake akizitaka pande hizo kuacha kuoneshana ubabe na badala yake wakae chini na kuzungumza. Kwenye eneo la SUKI, maneno ya…

Read More

Ezekiel Kamwaga   MIAKA michache iliyopita, Dorothy Semu – wakati huo akiwa Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, alianza kupokea simu; za kushawishi na kumtisha, kutaka akihame chama chake na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakati wa wimbi kubwa lililokuja kufahamika baadaye kama “kuunga mkono juhudi”. Waliokuwa wakiwasiliana naye, walimuahidi vyeo na mambo mengine. Wakati huo, Dorothy – sasa Kiongozi wa Chama (KC) cha ACT Wazalendo, alikuwa ameacha ajira ya utaalamu aliyosomea ya tiba ya viungo vya mwili (physiotherapy) na kujiingiza kindakindaki katika siasa. Ahadi ya vyeo, mamlaka na fedha, havikumbadilisha mawazo wala akili yake; katika…

Read More

Na Ezekiel Kamwaga KABLA ya kuandika kile nilichotaka kuandika, ni muhimu sana kuweka msingi. Na msingi wenyewe, kwa kukosa mifano ya karibuni sana, itabidi nirudi nyuma takribani miaka 365.  Mwaka 1659, kitabu cha Leviathan cha Thomas Hobbes kilichapwa kwa mara ya kwanza. Hoja yake kubwa ilikuwa kwamba wananchi wanatakiwa kuipa dola nguvu isiyo ya kawaida na mamlaka juu yao kwa malipo ya wao kuwa salama. Binadamu waliamua kuwa na serikali yenye viongozi wanaoishi kwa kuhudumiwa na umma kwa sababu moja kubwa, wananchi wawe salama. Wananchi wamekubali kujengwa kwa magereza, nchi kununua magari ya kuwasha, bunduki, virungu na silaha nyingine…

Read More

Picha: Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan akiteta na Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, Emmanuel Nchimbi, mara baada ya kupewa majukumu hayo mjini Zanzibar wiki hii. Picha kwa hisani ya CCM.  Na Ezekiel Kamwaga KUCHAGULIWA kwa Dk. Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu Mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumeibua swali moja kubwa kwa watu wengi; kwa nini  yeye? Tangu CCM kitangaze kwamba kimempa nafasi hiyo, nimeona wachambuzi na wadadisi wengi wakieleza na kujibu swali hilo la kwanza. Nimeamua kwamba sitajielekeza kujibu swali hilo na badala yake nitaangazia upande mwingine ambao haujajadiliwa sana kwenye mjadala mzima…

Read More

Na Ezekiel Kamwaga MWISHONI mwa wiki hii, nilikuwa na mjadala mzuri katika mojawapo ya makundi sogozi niliyopo. Rafiki yangu mmoja alijenga hoja kwamba tatizo la akinamama kujifungulia sakafuni lililotawala sana katika vyombo vya habari na mitandaoni hapa nchini au mwenendo wa suala la Naibu Waziri wa zamani wa Sheria na Katiba, Pauline Gekul, yasingetokea endapo hayati John Magufuli angekuwa bado Rais wa Tanzania. Kauli aliyotumia ilikuwa “Tutamkumbuka Magufuli”. Kauli ile ilinirudisha nyuma kidogo. Sikutaraji kwamba mtu wa aina ya huyo rafiki yangu angeweza kutoa sentensi nyepesi ya aina ile. Kuna sababu kubwa mbili za mimi kusema hivyo. Moja…

Read More

Na Ezekiel Kamwaga MWAKA 2017 alijitambulisha kupitia tamthilia ya Kapuni iliyorushwa na kituo cha DSTV. Tangu wakati huo, Leah Richard Mwendamseke, amekuwa akifyatua tamthilia ambazo zimekuwa sehemu ya maisha ya Watanzania – sasa akitamba na ile ya Jua Kali. Kwa wengi, Mwendamseke ni alama ya tamthilia za Kitanzania na safari yake haikuwa rahisi. Yeye ni mwongozaji wa tamthilia katika tasnia ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ikitawaliwa na wanaume. Kufika hapa tulipo, ambapo mchango wa sekta ya sanaa na burudani umeanza kuonekana hata katika bajeti ya serikali, Lamata kafanya kazi kubwa. Huu ni mwaka mwingine ambao Leah amezidi kujidhihiri kama mwongozaji…

Read More

Na Ezekiel Kamwaga NAMBA zinazungumza kuliko maneno. Mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan, alimteua Gilead Teri, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Wakati anapewa nafasi hiyo, wastani wa miradi ya uwekezaji iliyokuwa inarekodiwa na kituo hicho kwa miaka mitatu ya nyuma ilikuwa takribani 56. Katika mwaka wake wa kwanza tu, miradi imefika 158 – takribani mara tatu ya wastani wa miaka mitatu kabla yake. Si Watanzania wengi walikuwa wanamfahamu Teri kabla ya majukumu yake mapya. Kimsingi, kitabia, kituo hicho kilikuwa kinaongozwa na watumishi waandamizi wa serikali waliolelewa na kukulia kwenye mifumo hiyo. Mifano mizuri zaidi…

Read More

Na Ezekiel Kamwaga INGAWA kitaaluma ni mchumi, Profesa Adolf Mkenda, amejipambanua katika mwaka huu kama mwanasiasa anayetaka kuona mabadiliko kwenye sekta ya elimu ili iendane na changamoto za kisasa nchini na kimataifa. Kuanzia mwakani, Wizara ya Elimu imeandaa mitaala mipya ambayo itawafanya wahitimu kuwa na maarifa zaidi na uwezo mkubwa zaidi wa kukabili changamoto za kimaisha za kisasa ikiwemo elimu ya ufundi stadi. Mojawapo ya mabadiliko makubwa itakuwa ni kufanya elimu ya msingi kuwa miaka sita badala ya sasa huku ile ya awali ikiwa miaka miwili. Kama msomi, Mkenda anafahamu ubaya wa kuongoza taifa lenye wasomi wasiopikwa kukabili changamoto za…

Read More

Na Ezekiel Kamwaga MWAKA 2023 umeshuhudia Tanzania ikipewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yaliyopangwa kufanyika mnamo mwaka 2027. Tanzania itaandaa mashindano hayo kwa ushirikiano wa pamoja kati yake na jirani zake wa Kenya na Uganda. Hata hivyo, hakuna shaka kwamba Tanzania ndiyo hasa ilifanikisha ushindi huo. Siri ya ushindi huo iko kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia. Chini ya uongozi wake, heshima ya soka la Tanzania imepaa katika kiwango ambacho hakikufikirika hata miaka 10 tu iliyopita. Chini ya uongozi wake, Tanzania imeshiriki AFCON mara…

Read More