Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
Author: Ezekiel Kamwaga
Picha: Dk. Wilbrod Slaa. Kwa hisani ya The Citizen Na Ezekiel Kamwaga MWAKA 2015, akiwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mmoja wa wanasiasa wanaoheshimika sana nchini Tanzania, Dk. Wilbrod Slaa, alitangaza kupingana na hatua ya chama chake kumkaribisha Edward Lowassa kwenye chama hicho na kumfanya kuwa mgombea urais kwenye uchaguzi wa mwaka huo. Katika hotuba ambayo baadaye ilikuja kujulikana kwa jina la “Asset au Liability”, Dk. Slaa alihoji kama ujio huo wa Lowassa ni faida au hasara kwa chama hicho na kwamba kwa kuzingatia rekodi ya nyuma ya Waziri Mkuu huyo wa…
Picha: Rais Paul Kagame. Kwa hisani ya tovuti ya PML Daily Na Ezekiel Kamwaga All warfare is deception. Sun Tzu, The Art of War MOJAWAPO ya habari kubwa katika eneo la Afrika Mashariki mwezi huu ilikuwa ni mabadiliko makubwa kwenye sekta ya Ulinzi na Usalama yaliyotangazwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda mwanzoni mwa mwezi huu. Kwenye mabadiliko hayo, vigogo kadhaa wa sekta hizo walibadilishwa majukumu na wengine kuondolewa kabisa katika nyadhifa zao. Mtandao wa Al Jazeera katika taarifa yake ulieleza kwamba “siku moja baada ya kumteua waziri mpya wa Ulinzi na Mkuu Mpya wa…
Picha: Leila Sheikh Khatib Na Mohamed Said WASOMAJI wangu, niruhusuni niweke meseji niliyomtumia Leila Sheikh tarehe 12 December 2022. (Mtaniwia radhi nimeifanyia uhariri kidogo ili ipate kueleweka kwa wasomaji). Wakati huo CCM na serikali yake walikuwa katika pilikapilika ya kuandaa tamasha la kumuadhimisha Bi. Titi Mohamed. Maofisa wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo wakanitembelea nyumbani kwangu kwa kunialika Ikwiriri, Rufiji ambako ndipo kutakapokuwa na shughuli yenyewe na pia kurekodi kipindi cha radio na televisheni. Meseji yenyewe ilisomeka hivi; “Bi. Leila, Asalaam Aleikum Warahmatullah Wabarakatuh. Leo nilitembelewa na wataalamu kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na…
Picha: Sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam Na Ahmed Rajab KUMEKUWA na mijadala ya kushangaza nchini Tanzania tangu ibainike kwamba serikali yake inawasilisha bungeni Azimio la kujadili mkataba unaotarajiwa kutiwa saini baina yake na kampuni ya kimataifa ya DP World inayomilikiwa na serikali ya Dubai. Kiini cha mkataba huo ni Bandari ya Dar es Salaam na nyinginezo zilizo Bara ambayo kampuni hiyo inatarajiwa kuziendesha. Si dhamiri yangu kuujadili wala kuuhukumu huo mkataba. Sitofanya hivyo kwa sababu sikuuona na siyajui yaliyomo ndani yake. Naufata ule wasia maarufu wa Mao Zedong, aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Kikomunisti cha…
Na Ezekiel Kamwaga MWANAFALSAFA wa Ufaransa, Alexis de Tocqueville, alipata kunukuliwa akisema; “the most dangerous moment for a bad government is when it begins to reform itself” (wakati wa hatari zaidi kwa serikali isiyo ya kidemokrasia ni wakati ikianza kujirekebisha). Msomi huyo alikuwa anafanya uchambuzi wa nini kilisababisha Mapinduzi ya Ufaransa (1789 -1799) lakini kauli yake hiyo ina mantiki hadi leo. Usemi huo ndiyo msingi wa dhana ya revolution of rising expectation (mapinduzi kutokana na matarajio yaliyoongezeka) inayotumiwa sana na wataalamu wa sayansi ya siasa. Wakati fulani nilimsikia mbunge na waziri mstaafu, Profesa Anna Tibaijuka, akiizungumzia bungeni…
Maelezo ya Picha: Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, akiongoza kikao cha mazungumzo ya Kamati ya Maridhiano ya Zanzibar kilichofanyika Ikulu ya Zanzibar hivi karibuni. Picha kwa Hisani ya Ikulu ya Zanzibar Na Ezekiel Kamwaga WAKATI Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ikiwa inatimiza nusu muhula tangu iundwe baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, bado kuna sura ya mkanganyiko na kutoaminiana miongoni mwa vyama viwili vinavyounda serikali hiyo – ingawa uwepo wake peke yake unatoa matumaini ya kufikiwa kwa maridhiano ya kitaifa visiwani Zanzibar. Miaka miwili iliyopita, SUK ilipata pigo kutokana na kifo cha aliyekuwa…
Picha kwa hisani ya Gazeti la JAMHURI. Na Ezekiel Kamwaga KATIKA moja ya mikutano ya karibuni kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na wabunge wa Bunge la Tanzania, mmoja wa wabunge alisimama na kuzungumza maneno ya kumhakikishia Rais kwamba kwa mujibu wa mila na desturi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) suala la urais wake mwaka 2025 halina shaka na kwamba hakutakuwa na wa kumpinga. Baada ya kumsikiliza, Rais Samia aliamua kumjibu hapohapo kwamba “Kama mtataka kunipa urais kwa sababu ya mila na desturi na si kwa sababu ya kutimiza majukumu yangu ipasavyo, ni afadhali…
Maelezo ya picha. Mwandishi wa makala haya, Ahmed Rajab (kushoto), akisalimiana na Abu Mahdi al Muhandis, aliyekuwa Kaimu wa Mkuu wa Jeshi la Mgambo la al-Hashd al-Sha‘abi nchini Irak mnamo mwaka 2017. Na Ahmed Rajab MWANZONI mwa Oktoba, 2017, nilialikwa kuhudhuria mkutano jijini Baghdad, Iraq, kuujadili ugaidi wa kimataifa. Baada ya kuisoma barua ya mwaliko, akili yangu ilizileta machoni mwangu kumbukumbu za miaka tisa kabla ya hapo. Nilijikuta Dubai nikiwa mkuu wa chumba cha habari cha IRIN, Shirika la Habari la siku hizo la Umoja wa Mataifa. Tulikuwa na dhamana ya kukusanya, kuhariri na kuchapisha ripoti na…
Picha: Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume. Na Ahmed Rajab MENGI yameandikwa na mengi yataendelea kuandikwa kumhusu Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa mwanzo na wa pekee wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambaye Aprili, 26, mwaka 1964 alikubali kuiunganisha nchi yake na ile ya Tanganyika. Hadi sasa walioandika kumhusu Karume ni waandishi wa habari, wanahistoria na wataalamu wa fani ya sayansi ya siasa. Waandishi wa riwaya hata wa riwaya sahili na wa tamthilia bado hawajajitokeza uwanjani kumuandika Karume. Sitoshangaa pakitokea magwiji wa tanzu hizi mbili za fasihi watakaoamua kumtoa ukumbini Sheikh Karume…
Maelezo ya picha: Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mamilionea wa Tanzania baada ya mkutano wa Kamati ya Okoa Maisha Somalia uliofanyika Ikulu mwaka 2011 kuhusu namna ya kuisaidia nchi ya Somalia kwa misaada ya kibinadamu. Kutoka kushoto ni Haruna Zakaria, Said Bakhresa, hayati Reginald Mengi, Kikwete, Gulam Dewji na Balozi Said Shamo. Na Ezekiel Kamwaga KWA mara nyingine tena, bilionea Aliko Dangote wa Nigeria ameonyesha njia barani Afrika kwa kufanya uwekezaji ndani ya taifa lake utakaookoa mabilioni ya fedha za kigeni ambayo nchi yake ingelipa kuagiza mafuta kutoka nje. Mradi wa…
