Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
Author: Ezekiel Kamwaga
Na Ezekiel Kamwaga MFANO mmoja unatosha kumueleza Waziri wa Mambo ya Nje, January Makamba, na utendaji wake tangu alipoingia kwenye wizara hiyo mwaka huu. Kwenye ndege wakati tukirejea Dar es Salaam kutoka India kwenye ziara ya kitaifa ya Rais Samia nchini humo, mmoja wa mawaziri alinieleza kwamba tangu awe waziri – ziara ile ilikuwa ndiyo imeandaliwa vizuri zaidi na Wizara ya Mambo ya Nje kuliko nyingine zote alizowahi kuwepo. Na alichosema kilikuwa na maelezo. Tangu January ateuliwe kwenye nafasi hiyo Agosti mwaka huu, kila ziara imekuwa na vitu kadhaa vya tofauti; kwanza ameanzisha utaratibu wa kutoa maelezo kuhusu ziara za…
Na Ezekiel Kamwaga MWANZONI mwa mwaka huu, Kiongozi wa Chama wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, alikuwa pengine mwanasiasa aliyekuwa akishambuliwa zaidi mitandaoni kuliko mwingine. Mashambulizi hayo yalitokana na ushiriki wake katika Kikosi Kazi kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mapitio ya sheria za uchaguzi zilizopo nchini. Kikosi kazi hicho hakikuwa kinaungwa mkono na chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kwa sababu zake na kuwa kwake kwenye timu hiyo, halikuwa jambo rahisi kisiasa kwake. Kimsingi, ACT Wazalendo chini ya uongozi wake, kiliunga mkono ajenda ya maridhiano ya kisiasa ya Rais Samia kuanzia siku ya kwanza. Ni kazi ya kikosi hicho…
Na Ezekiel Kamwaga SIKU moja tukiwa New Delhi, India, kwenye ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, alifanya mkutano na waandishi wa habari wa Tanzania tuliokuwa pale. Nakumbuka alipomaliza mkutano, nilikwenda kumshika mkono na kumkumbatia, nikamueleza kwamba nimefurahi kwa kilichotokea. Bashe alikuwa ametoka kueleza waandishi wa habari kuhusu makubaliano ya Tanzania na India kwenye biashara ya mbaazi na korosho ambayo ikifanyika, nchi yetu itaingiza mabilioni ya shilingi. Wakati ule kulikuwa na mjadala mkubwa nchini kuhusu umuhimu wa ziara za viongozi nchi za nje na dili na India ilikuwa na thamani kubwa kuliko ziara zote za viongozi…
Na Ezekiel Kamwaga MAJUZI nilihudhuria harusi moja jijini Dar es Salaam na wakati muda wa kwenda kula ulipofika, MC akatania “wakati tunapokwenda kupakua chakula, msisahau ushauri wa Profesa Janabi”. Ukumbi mzima ulilipuka kwa vicheko. Ni kama kila mtu alikuwa anamjua Profesa Mohamed Janabi na ujumbe wake kwa jamii yake. Kwa hakika, katika mwaka 2023, hakuna mwanataaluma wa Kitanzania ambaye amejulikana kazi yake na kugusa maisha ya watu kumzidi Profesa Janabi. Mkurugenzi Mtendaji huyu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) amejipambanua kwa mafunzo na ushauri wake kuhusu umuhimu wa watu kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanayoharibu maisha ya Watanzania…
Picha: Daniel Godfrey Chongolo. Kwa hisani ya tovuti ya CCM. Na Ezekiel Kamwaga WIKI mbili zilizopita, mmoja wa rafiki zangu ambaye ni kiongozi serikalini, alikuja Dar es Salaam kikazi. Katika mazungumzo yetu tulipoonana, suala la kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, lilichukua sehemu kubwa ya mazungumzo yetu. Ni sadfa kwamba mimi na rafiki yangu huyo tunafahamiana pia na Chongolo. Jambo moja aliloniambia na limebaki kwenye kumbukumbu zangu ni kuwa; “kwa sasa, sina sababu ya kukubali kuwa Katibu Mkuu wa CCM kama chama kitataka kuniteua kushika wadhifa huo”. Kwa nini…
Na Ezekiel Kamwaga OKTOBA mwaka huu, nilikuwa sehemu ya waandishi wa habari wa Tanzania waliokuwa kwenye ziara ya kitaifa ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Zambia. Ingawa vyombo vyetu vya habari viliandika kuhusu masuala makubwa yaliyotokea huko, jicho langu lilivutwa na jambo lingine dogo nililoshuhudia. Oktoba 24, nilipata fursa ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Zambia zilizofanyika katika Ikulu ya Lusaka. Kila kitu kilikuwa tofauti kwangu na nilijifunza mawili matatu kutoka pale na ndiyo msingi wa makala haya ya leo. Muktadha ni muhimu. Mimi nimezaliwa na kukulia katika eneo la Kurasini, Temeke. Mojawapo ya…
Na Ezekiel Kamwaga DANIEL Godfrey Chongolo amemaliza muhula wake kama Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuandika barua ya kujiuzulu na kuhitimisha takribani miaka miwili na miezi saba ya kutumikia nafasi hiyo. Wakati alipotangazwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, si watu wengi walikuwa wamewahi kumsikia kabla – ingawa aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya za Longido na Kinondoni, lakini pasi na shaka, sasa hakuna ambaye hajawahi kumsikia. Ni muhimu nikaeleza mapema kwamba Chongolo ni mtu ninayefahamiana na kuheshimiana naye na kwa hakika sijafurahishwa na namna na aina ya mashambulizi yaliyoelekezwa kwake katika siku za mwisho za uongozi…
Na Ezekiel Kamwaga “Maji kila mahali lakini hakuna hata tone moja la kunywa” Samuel Taylor Coleridge, The Rime of the Ancient Mariner MWANZO kabisa, napenda kutoa pole kwa Watanzania wenzangu ambao wameathirika kwa namna moja au nyingine na mvua hizi za El Nino zinazoendelea kunyesha. Ninafanya kazi kwenye kituo cha televisheni na ninaona picha nyingi za maeneo tofauti ya Tanzania ambako watu wameathirika na mvua. Nimezaliwa, kukulia na bado naishi Dar es Salaam na hivyo nimeshuhudia pia kwa macho yangu kile kinachoendelea sasa kufuatia mvua zinazonyesha. Ukweli mmoja wa wazi kuhusu Dar es Salaam, na Tanzania…
Picha: John Heche (kwa hisani ya mtandao wa Millard Ayo) Na Ezekiel Kamwaga MWAKA 2016 utabaki kuwa na historia ya kipekee kwenye miaka ya karibuni na pengine mingi inayokuja. Huu ndiyo mwaka ambapo neno moja lilitajwa kuwa neno lililotumika zaidi katika lugha za Kijerumani na Kihispania mtawalia; Postfaktisch na Posverdad. Kwenye Kiingereza, linajulikana kama Post-Truth. Neno hili lina maana ya nyakati ambazo ukweli unawekwa kapuni na badala yake siasa zinatawaliwa na mambo yaliyo rahisi kugusa hisia za watu. Si ajabu kwamba matumizi ya neno hili yalikuja sambamba na ujio wa Donald Trump kama Rais wa Marekani. Chukulia…
Picha: Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) akizungumza baada ya kupokewa katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma mara baada ya kurejea nchini akitokea nchini Angola alikoshinda uchaguzi wa taasisi hiyo ya mabunge duniani. Picha kwa hisani ya mtandao wa Zanzinews. Na Ezekiel Kamwaga WAKATI Ikulu ilipotoa taarifa Septemba 14 mwaka 2015 kuwa Rais Jakaya Kikwete amemteua Mhadhiri wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Tulia Ackson, kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wengi walipokea taarifa hiyo kwa mshangao. Sababu kubwa zilikuwa mbili; mosi kwamba kwa nini…
