Author: Ezekiel Kamwaga

Na Ezekiel Kamwaga Katika moja ya hotuba zake maarufu za zamani, Baba wa Taifa la Zambia, Dk. Kenneth Kaunda, alipata kuelezea uhusiano baina ya taifa lake na Tanzania kuwa sawa na ule wa pacha walioungana. Hakuna kilichokuwa kinaeleza uhusiano huo kama uhusiano baina yake na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Wawili hawa walipendana kiasi kwamba Kaunda aliamua kumpa mmoja wa watoto zake jina la Kambarage – ambalo ni moja ya majina ya Mwalimu Nyerere. Na hata wakati alipokuwa akipita katika wakati mgumu kwenye utawala wa mbadala wake, Frederick Chiluba, kiasi cha kususa kula, ni Mwalimu ndiye…

Read More

Na Ezekiel Kamwaga NIANZE kwa kutumia takwimu kueleza kile nilichopanga kuandika kwenye makala haya. Katika siku nne ambazo Rais Samia Suluhu Hassan alikaa nchini India, Oktoba 8 mpaka 11 mwaka huu, kuna siku mbili ambazo jina lake liliongoza kwa kusakwa kupitia mitandaoni na raia wa taifa hilo. Siku ya kwanza ilikuwa Oktoba 9 na kisha Oktoba 10 hali ikawa hivyo. Kama isingekuwa kuwepo kwa mechi ya mchezo wa Kriketi baina ya Pakistan na Sri Lanka Oktoba 8, kuna kila dalili kwamba huenda Rais Samia angekuwa namba moja. Nchini India, kriketi inapendwa pengine kuliko hata Watanzania wanavyopenda…

Read More

Na Ezekiel Kamwaga RAIS Yoweri Museveni wa Uganda alipata kuulizwa wakati mmoja kuwa ni jambo gani kubwa analodhani Baba wa Taifa la Tanzania, Julius Nyerere, alilifanya kiasi cha kubaki madarakani kwa muda mrefu? Pasi na kufikiri sana, Museveni alijibu; “He tamed the army” Kwa tafsiri ya haraka ya lugha ya Kiswahili, alimaanisha alilidhibiti Jeshi. Wakati tukiadhimisha Kumbukizi ya Baba wa Taifa hii leo, jibu hilo la Museveni limerudi tena kichwani kwangu. Na limerudi kwa sababu kuliko katika wakati mwingine wowote tangu nimekuwa mtu mzima, Afrika inapitia katika kipindi ambacho Mapinduzi ya Kijeshi yameanza tena kuwa fasheni. Na…

Read More

Picha: Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere akiwa na Dk. Salim Na Ezekiel Kamwaga   KWENYE tukio la uzinduzi wa Makavazi ya Dk. Salim Ahmed Salim jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, Profesa Said Yahya Othman aliuliza swali gumu kwa wazungumzaji watatu katika tukio lile; kuhusu ubaguzi ulio wazi katika siasa za Tanzania. Kama mwanazuoni, Profesa Saida alizungumzia kuhusu rangi. Akasema inaonekana katika Tanzania kuna rangi zinafutika na kusahaulika lakini kuna rangi moja haifutiki – nyekundu, inayohusishwa na kilichokuwa kikifahamika kama Chama cha Hizbu. Dk. Salim aliwahi kuwa mwanachama wa Hizbu zaidi ya miaka 60 iliyopita. Uhusiano wake…

Read More

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa tukio la kuapisha mabalozi na watendaji wengine wa serikali lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam wiki hii. Picha ya Ikulu   Na Ezekiel Kamwaga KUELEWA uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kumfanya Boniface Gissima Nyamo-Hanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la TANESCO kunahitaji tafakuri ya mambo kadhaa yanayohusu shirika hilo na historia ya miaka ya karibuni ya mhusika. Labda nianze na jambo ambalo halijasemwa sana. Kwamba katika uteuzi wa wiki iliyopita wa Rais Samia, watu watatu; Nyamo-Hanga, Mkurugenzi Mtendaji wa TTCL, Peter Ulanga na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,…

Read More

Picha: Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko (kulia), akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, katika mojawapo ya matukio ya kiserikali hivi karibuni. Na Ezekiel Kamwaga DESEMBA 30, mwaka 1978, mapacha walizaliwa katika familia moja ya wakulima huko Bukombe. Wazazi hawakuwa na uwezo wa kuhudumia mapacha hao peke yao huku wakiendelea na shughuli zao za kutafuta riziki kama kawaida; ikabidi jukumu la kuwalea liangukie kwa dada wa mapacha hao. Huyu ndiye dada ambaye ilibidi akatishwe maisha yake ya shule ili hatimaye Kulwa na Doto Biteko – Naibu Waziri Mkuu mpya wa Tanzania, wapate mtu wa kuwalea.…

Read More

Picha: Sehemu ya umati wa wananchi  waliojitokeza kwenye mazishi ya Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Kigoma, Abbas Idi Noboka, Agosti 29, 2023. Picha kwa hisani ya Zitto Kabwe.  Na Zitto Kabwe Sheikh Abbas Idi Noboka, Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Kigoma, Mjumbe wa Baraza la Masheikh Mkoa na Sheikh wa Kata ya Mwanga alifariki dunia mnamo Agosti 28, 2023 na kuzikwa  siku moja baadaye katika makaburi ya Lubengera yaliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji. Sheikh Abbas aliugua kwa muda mfupi na kufanyiwa operesheni ya kukata utumbo. Baada ya operesheni alipata shinikizo kali la moyo ( massive heart attack) na…

Read More

Picha: Sheikh Vuai Kitoweo, aliyekuwa Rais wa Chama cha Hizbu. Picha kwa hisani ya Ahmed Rajab Na Ahmed Rajab KATIKA mwezi wa Machi hali ya hewa jijini Accra, Ghana, huwa inaudhi bila ya kiasi kwa joto linavyokuwa kali. Jioni ndipo huzidi kushtadi.  Nadra mvua kunyesha. Siku moja Machi 1958, saa za Magharibi, wakombozi wawili wa Kiafrika walikaa, gilasi mkononi, wakipunga upepo kwenye baraza ya hoteli ya Avenada, iliyokuwa ikimilikiwa na Mgiriki. Upande mmoja alikuwa Sheikh Ali Muhsin Barwani kutoka Zanzibar na aliyemkabili alikuwa Mwalimu Julius Nyerere kutoka Tanganyika.  Nyerere alikuwa rais wa chama kikuu…

Read More

Rais Samia Suluhu Hassan akimwapisha Ali Idi Siwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) wiki hii. Picha kwa Hisani ya Ikulu Na Ezekiel Kamwaga MARAIS huwa hawachagui siku au mazingira yatakayowafanya washike wadhifa huo katika wakati husika. Kama ungekutana na Ali Hassan Mwinyi mwaka 1983 na kumueleza angekuwa Rais wa Tanzania mwaka 1985, pengine angekushangaa. Hadi Januari mwaka 2015, wengi walidhani ni ndoto za mchana kwa John Magufuli kuwa Rais wa Tanzania. Lakini wote walikuja kuwa marais. Rais Samia Suluhu Hassan hakupanga kuwa Rais wa Tanzania mnamo Machi mwaka 2021. Hakuchagua…

Read More

Na Ezekiel Kamwaga KUELEKEA kipindi cha Kwaresma na Sikukuu ya Pasaka ya mwaka 2018, Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (TEC) lilitoa waraka ambao kimsingi ulikosoa vitendo vya uminyaji wa demokrasia na uhuru wa watu kujieleza uliokuwepo wakati wa utawala wa hayati Rais John Magufuli. Waraka ule ulikuwa na sehemu nne lakini sehemu iliyozua mjadala zaidi ilikuwa ni sehemu ya tatu iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho; “Dalili za Nyakati Zetu Tanzania” ambapo pamoja na mambo mengine, Maaskofu walieleza kutofurahishwa kwao na maandamano na mikutano ya kisiasa kuzuiwa na vyombo vya dola huku vyombo vya habari vikifungiwa.…

Read More