Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
Author: Ezekiel Kamwaga
Na Peter Nyanje KATI ya mambo yaliyoibuka kwa hisia kali kwenye mjadala wa uwekezaji katika bandari nchini ni suala la Muungano. Ingawa hivi sasa hoja hii inaonekana kama imekufa pengine kwa sababu haikuwa katika kiini cha mjadala yaani vifungu vya mkataba, lakini hisia zilizotolewa kwenye kulijadili suala hilo zimeacha makovu ambayo pengine ni makali zaidi kuliko makovu kwenye Muungano yaliyopata kuachwa huko nyuma. Hisia hizo ziliibuliwa na kauli ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ambaye, pamoja na mambo mengine, alihoji kwa nini bandari za Zanzibari hazikuhusika katika mkataba huo wakati bandari…
Na Ezekiel Kamwaga KIFO cha Jecha Salim Jecha kilichotokea jijini Dar es Salaam jana, kimemuondoa duniani mtu ambaye – kwa miaka mingi inayokuja, jina lake litanasabishwa na Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2015 ambao – kinyume na matarajio ya wengi na sheria za uchaguzi za visiwa hivyo, matokeo yake yalifutwa. Jecha ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) wakati wa uchaguzi huo na yeye ndiye aliyetangaza kufutwa kwa matokeo hayo akitoa sababu za kuwepo kwa kasoro mbalimbali – hasa kisiwani Pemba, ilikokuwa ngome ya chama kikuu cha upinzani Zanzibar wakati huo; Chama…
Na Ezekiel Kamwaga MWAKA 1978, Rais Julius Nyerere, alilazimika kufanya uamuzi mzito wa kuiingiza Tanzania vitani dhidi ya Uganda. Majeshi ya Nduli Idi Amin yalikuwa yameivamia ardhi ya Tanzania na kama Amiri Jeshi Mkuu, Baba wa Taifa hakuwa na namna zaidi ya kupeleka majeshi yetu yaende vitani akijua kuna watu wanakwenda kupoteza maisha yao kwa sababu hiyo. Huo ndiyo mzigo wa uongozi. Nimeisoma na kusikiliza mara kadhaa hotuba yake ya kutangaza vita hiyo aliyoitoa Novemba 2, 1978 na kumbukumbu ya kudumu ya vita ile inahusu maneno haya maarufu; “Uwezo wa Kumpiga Tunao, Sababu ya Kumpiga Tunayo na…
Picha: Picha ya pamoja kati ya Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye na kiongozi wa chama cha upinzani cha CNL, Agathon Rwasa (kulia). Picha ya Al Jazeera: Ezekiel Kamwaga RIPOTI maarufu ya Taasisi ya Kimataifa ya ACCORD ya mwaka 2016 iliyoitwa Conflict in the Great Lakes Region, ilieleza kwa kifupi kwamba vita na migogoro isiyokwisha katika eneo la Maziwa Makuu vinasababishwa na uwezo mdogo wa serikali za nchi hizo kudhibiti misuguano ya kijamii inayosababishwa na tofauti za kikabila, ugawaji mbaya wa rasilimali ardhi na kutengwa kisiasa kwa makundi fulani ya kijamii. Katika eneo hili la Nchi za Maziwa Makuu,…
Picha: Kiongozi wa Upinzani nchini Burundi, Agathon Rwasa, akizungumza na Mhariri wa Gazeti la Dunia, Ezekiel Kamwaga, katika mahojiano maalumu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Picha ya Maktaba. Na Ezekiel Kamwaga KIONGOZI wa chama cha upinzani cha Congress for National Liberty (CNL) nchini Burundi, Agathon Rwasa, amesema chanzo kikubwa cha migogoro ya kisiasa barani Afrika ni viongozi kutofahamu nini hasa maana ya nchi kuwa huru. Katika mahojiano maalumu aliyofanya na Gazeti la Dunia (GD) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, Rwasa alisema tatizo hilo limeanzia tangu kizazi cha viongozi wa kwanza baada…
Picha: Picha ya pamoja ya Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, na Balozi na Waziri Mstaafu, Ali Karume. Kwa Hisani ya Jambo TV. Mzingile ni tafsiri ya Kiswahili ya neno labyrinth Na Ezekiel Kamwaga SAKATA la mwanasiasa na mwanadiplomasia mwandamizi wa Zanzibar, Ali Karume, kufukuzwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) limeibua swali moja kubwa kwa wafuatiliaji wa siasa za visiwani humo; Nini kinaendelea? Balozi Karume si mwanasiasa wa kawaida wa Zanzibar. Yeye ni mtoto wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) lakini pia ni mdogo wa aliyepata kuwa Rais wa SMZ, Amani Karume.…
Sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam. Picha ya gazeti la serikali la Daily News. Na Ezekiel Kamwaga KAMA kuna kitu ambacho mjadala kuhusu uwekezaji unaopangwa kufanywa kwenye bandari za Tanzania na kampuni ya DP World kutoka Dubai umefanikiwa kufanya ni kufichua kuhusu uwezo, hulka na silka za Watanzania – hasa wale wenye ushawishi au mamlaka katika jamii yetu. Kimsingi, makundi makubwa manne yalijionyesha bayana kupitia mijadala na mazungumzo yaliyodumu kwa takribani mwezi mmoja; kundi la wale walioamua kuunga mkono tu bila kuhoji chochote, waliopinga tu – wakati mwingine wakipotosha makusudi au kuendeleza hoja ambazo zina majibu,…
Wakili Rugemeleza Nshala. Picha kwa hisani ya Katiba TV Na Ezekiel Kamwaga MARA nyingi huwa nafanya rejea kupitia maandishi ya hayati Profesa Samuel Huntington wa Marekani. Katika kitabu chake cha mwaka 1993, The Third Wave: Democratization in the Late Twentieth Century, msomi huyu alieleza kwa undani kuhusu ni wakati gani unaweza kubashiri mwisho wa utawala uliodumu madarakani kwa muda mrefu. Mojawapo ya dalili za mwisho wa utawala unaoelekea ukingoni – kwa mujibu wa Huntington, ni mgawanyiko wa dhahiri miongoni mwa tabaka la watawala. Ukianza kuona wale walioshika hatamu wakiwa wanagawana mbao, ujue mchezo umekwisha. Hivyo, Yoweri…
Picha: Rais William Ruto. Kwa Hisani ya BBC Na Paul Sewe UCHAGUZI Mkuu wa Kenya uliofanyika mwaka jana ulimalizika kwa ushindi wa Rais William Ruto na aliyekuwa mgombea mwenza wake, Rigathi Gachagua. Sasa miezi tisa imepita tangu ushindi wao huo lakini bado kuna maswali kuhusu mwelekeo ambao serikali yao imeamua kuchukua. Ni vigumu sana kupata mtu anayeitakia nchi yake maovu tu ila kuna nchi zinazochosha kuzitakia mema, maana yote wanayofanya wenye dhamana ya kuendesha nchi ni maovu tu. Duniani kote sasa hivi kuna changamoto za kiuchumi na taifa la Kenya halijapona kwenye changamoto hizo. Kama…
Picha: Hayati Rais John Magufuli akisalimiana na Edward Lowassa katika mojawapo ya matukio ya kitaifa. Picha ya Ikulu Na Ezekiel Kamwaga MAJUZI nilikuwa nasikiliza Podcast ya The Rest is Politics kutoka nchini Uingereza na mada iliyozungumzwa ilinivutia. Watangazaji wa kipindi hicho, Alastair Campbell na Rory Stewart waliulizana swali moja; Kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1997 nchini kwao, Tony Blair alishinda uchaguzi au John Major alishindwa? Mwishoni walikubaliana kwamba Tony alishinda uchaguzi ule kwa sababu kwa mazingira ya wakati ule yalivyokuwa, haingekuwa rahisi kwa Major kushinda. Ni bahati nzuri pia kwamba kwenye mahojiano ya wawili hao na Major…
