Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
Author: Ezekiel Kamwaga
Na Ezekiel Kamwaga MUONGO mmoja uliopita, nilikuwa na mazungumzo na mmoja wa maofisa waandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ofisini kwake na mara akapita mtu mmoja wa makamo mbele yetu. Rafiki yangu akaniuliza “unamfahamu yule”, nikajibu hapana. Akanitajia jina la Khamis Mussa Omar, wakati huo akiwa Mjumbe wa Bodi ya BoT, na kwa maelezo ya ofisa huyo, kama angeambiwa ataje Wazanzibari mahiri watatu aliopata kukutana nao, Khamisi angekuwa mmoja wao. Huyu ndiye Khamis ambaye wiki iliyopita alitangazwa na Ikulu kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini China. Kwa wanaomfahamu mtumishi huyu wa serikali kwa zaidi ya miaka…
Picha: Sehemu ya matukio yaliyotokea nchini Tanzania kama yalivyoripotiwa kwenye magazeti ya Agosti 16, 2023. Picha kwa hisani ya mtandao wa Millard Ayo. Na Ezekiel Kamwaga KUTOKANA na hali ya Tanzania inayoendelea hivi sasa – hasa katika medani ya siasa, jambo moja ambalo nimelibaini ni kuwa ni kwa kiasi gani umoja wetu kama taifa bado ni nyondenyonde na unahitaji kufanyiwa kazi. Ni rahisi kuona kwa nje taifa lenye amani na utulivu kwa takribani miaka 60 sasa, lakini kwa ndani, nimeanza kuona nyufa za taifa lililo hatarini. Ni muhimu nikakiri kwamba kwa mara ya kwanza katika maisha yangu…
Picha: Rais mstaafu, Jakaya Kikwete. Picha kwa hisani ya gazeti la Daily News. Na Godfrey Dilunga NJAA ya wadokozi ambao siku hizi ni maarufu kwa jina la mafisadi, imegharimu kwa kiasi kikubwa maisha ya raia wa kawaida nchini. Kodi anayolipa raia huyo kwa mfano, wakati anaponunua chumvi au sukari dukani imekuwa ikidokolewa na mafisadi kwa kipindi kirefu sasa. Kodi hiyo imekuwa ikidokolewa na kwa kutumia mbinu za kifisadi, imekuwa ikigharimia miradi ambayo mwishowe hunufaisha mafisadi. Miradi kama ya kuzalisha umeme wa dharura, ununuzi wa rada ya kijeshi kwa bei ya juu na hata ununuzi wa ndege ya…
Picha: Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe. Picha kwa hisani ya Gazeti la Mwananchi Na Ezekiel Kamwaga MWANZONI mwa wiki hii, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, alitangaza Baraza Kivuli la Mawaziri la chama hicho lenye wajumbe 54 litakalokuwa na wajibu wa kusimamia na kuzungumzia utendaji wa serikali katika sekta tofauti za masuala yanayogusa maisha ya Watanzania. Umekuwa ni utaratibu wa chama hiki kuunda baraza kivuli tangu kuasisiwa kwake takribani miaka tisa iliyopita. Hata hivyo, kulinganisha na miaka mingine, nimeliona baraza la safari hili likiwa tofauti kwa maana ya muundo wake,…
Picha: Chen Boda, aliyepata kuwa “Top Pen” wa Chama cha Kikomunisti cha China. Picha kwa hisani ya Memoires de Guerre Na Ahmed Rajab SI kwamba najaribu kujipendekeza kwa muasisi na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Dunia ambaye siku hizi amejipa lakabu ya ‘Top Pen’. Lakini nataka kuyaanza makala haya kwa kusema kwamba kati ya lakabu ambazo Ezekiel Kamwaga amejipa hii ya ‘Top Pen’ ndiyo yenye kumsibu. Kabla ya kuitumia lakabu hiyo Kamwaga alijibandika lakabu mbili nyingine ninazozikumbuka: ‘The Sunak’ na baadaye ‘The Wolf’. Amenambia mwenyewe kwamba aliipachika lakabu ya Sunak katika majina yake baada ya Rishi…
Picha: Mwandishi wa makala haya, Ezekiel Kamwaga, akihojiwa na Shirika la Utangazaji wa Rwanda kama sehemu ya jopo la waandishi wa habari wa nchi mbalimbali za Afrika walioripoti kuhusu Uchaguz Mkuu wa Rwanda wa mwaka 2017. Picha ya Maktaba Na Ezekiel Kamwaga UMEWAHI kujiuliza ni kwa namna gani makundi mbalimbali ya waasi huwa wanaishi wanapokuwa msituni wakiishi kusubiri kupindua serikali zilizo madarakani? Nimekuwa najiuliza swali hili kwa muda mrefu na majibu niliyapata nchini Rwanda hivi karibuni. Nkomeje Jean Claude (36) mmoja wa waliokuwa waasi katika kundi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), alinipa sentensi moja…
Picha: Viongozi wa wanajeshi waliopindua serikali ya Niger wakitoa taarifa rasmi kwa wananchi kuhusu jambo hilo. Picha kwa hisani ya tovuti ya Al Jazeera Na Ahmed Rajab TANGU Jumatano iliyopita wakati Rais Mohamed Bazoum alipopinduliwa nchini Niger hadi leo Gazeti la Dunia linapoingia mtandaoni, hakuna mwenye hakika iwapo Niger imeponyoka kutoka mikononi mwa Ufaransa. Au ikiwa imebaki ikining’inia tu kwenye makucha ya huyo mkoloni wake wa zamani. Hata hivyo, ni wazi kwamba Ufaransa pamoja na Marekani zimepata pigo kubwa kwa kuangushwa kwa Bazoum. Kinachodhihirika ni kwamba sera za Ufaransa zinazohusiana na ukanda mzima wa nchi za Sahel…
Picha: Mwandishi wa taabini hii, Mohamed Said, akizungumza na swahiba yake, Sheikh Aly Basaleh, enzi za uhai wake, katika moja ya mazungumzo waliyofanya nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. Picha kwa hisani ya Mohamed Said Na Mohamed Said Nimepata taarifa ya kifo cha Sheikh Aly Basaleh msikitini petu Masjid Nur baada ya Sala ya Maghrib. Nilipofika nyumbani kitu cha kwanza nilichofanya ni kuingia Maktaba kutafuta kitabu alichoandika, ‘’Kwa Nini Waislamu Walalamika,’’ kilichotolewa na Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania. Nimekifunua kitabu na kusoma, ‘’Yaliyomo.’’ Kitabu hiki kina mengi yanayomfaa kila Muislam kuyajua, mambo ambayo…
Picha: Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Othman Masoud (kulia), akizungumza na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Dunia, Ezekiel Kamwaga, kwenye mahojiano maalumu ofisini kwake kuhusu tathmini ya Nusu Muhula wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) baina ya vyama vya CCM na ACT Wazalendo visiwani humo. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Na Ezekiel Kamwaga Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud, amesema kwamba uhusiano wake kikazi na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, ni mzuri na ndiyo umefanikisha kutopanda kwa joto la kisiasa visiwani humo…
Picha: Rais Samia Suluhu Hassan Na Ezekiel Kamwaga KUJENGA msingi wa hoja yangu kwenye makala haya, ni muhimu kurejea nyuma miaka minane iliyopita. Mwaka 2015, Tanzania ilifanya Uchaguzi Mkuu. Katika uchaguzi huo, vyama vya upinzani vilipata takribani asilimia 40 ya kura zote – zikiwa ni kura nyingi kuliko wakati mwingine wowote hapa nchini tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mnamo mwaka 1992. Katika uchumi, Tanzania ilikuwa moja ya nchi zilizojulikana kwa uimara wa uchumi wake, ukipanda kwa wastani wa walau asilimia sita karibu kipindi chote cha utawala wa Rais Jakaya Kikwete. Ni katika…
